SHEIKH MKOA WA SINGIDA: RAIS SAMIA KUCHANGIA UJENZI WA MSIKITI ISIWE NONGWA - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Tuesday, 18 June 2024

SHEIKH MKOA WA SINGIDA: RAIS SAMIA KUCHANGIA UJENZI WA MSIKITI ISIWE NONGWA

Sheikh wa Mkoa wa Singida, Issa Nasoro akizungumza na Waumini wa Dini ya Kiislamu (hawapo pichani) wakati wa ibada ya Eid Al-Adha iliyofanyika juzi.

........................................

Na Dotto Mwaibale, Singidani Blog.

SHEIKH wa Mkoa wa Singida, Issa Nasoro amesema Rais Samia Suluhu Hassan kuchangia Sh.Milioni 50 kwa ajili ya ukarabati wa Msikiti wa Taqwa uliopo mjini Singida isiwe nongwa kwani si mara ya kwanza kwa viongozi mbalimbali kufanya hivyo.

Akitoa hutuba wakati wa Sikukuu ya Eid Al- Adha iliyofanyika Msikiti wa Taqwa mjini Singida alisema kuna baadhi ya wanasiasa wameibuka na kudai kuwa eti Rais Samia ametoa hongo kwa Waislamu wa Mkoa wa Singida kwa kuwapa kiasi hicho cha fedha jambo ambalo ni kumdhalilisha kiongozi wa nchi.

Sheikh Nasoro alisema kuchangia michango mbalimbali ya madhehebu ya dini sio mara ya kwanza amekuwa akifanya hivyo hata katika makanisa sasa anashangaa kuona kwanini wanasiasa wanalalamikia mchango huo uliotolewa kwa waislamu wa Mkoa wa Singida.

Aidha, Sheikh Nasoro amewataka waislamu Mkoa wa Singida kutokubali kugawanywa na wanasiasa kutokana na vyama vyao vya siasa badala yake waendelee kuujenga uislamu wao.

Alisema kuna nchi nyingine wananchi wake wanashindwa kupata hata muda wa kuabudu kutokana na kukosekana kwa amani kulikosababishwa na wanasiasa hivyo aliwataka waislamu hasa vijana kutokubali vishawishi vyovyote ambavyo vinaweza kuhatarisha amani iliyopo ipotee na badala yake akawaomba vijana kuhakikisha amani hiyo inalindwa na kudumu na kujikita zaidi kuwalinda viongozi wa nchi.

Akizungumzia kuhusu iddi ya kuchinja (Eid Al- Adha alisema kila mwislamu anaweza kufanya hivyo akitolea mfano kuwa Mkoa wa Singida una maeneo makubwa ya ardhi wanaweza wakatengeneza eneo ambalo kila mwislamu akaweka mbuzi na ngombe kati ya mmoja hadi wawili na wakati wa chinja unapowadia nao wakaenda kufanya ibada hiyo hata nje ya nchi kwani jambo hilo lipo ndani ya uwezo wao badala ya kutegemea wageni kutoka Uturuki na maeneo mengine kuja kuwafanyia.

Sheikh wa Mkoa wa Singida, Issa Nasoro akizizitiza jambo katika swala hiyo.

Waumini wa dini ya Kiislamu wakiwa kwenye swala hiyo.
Ustadhi Is-haka Hassan akitoa hutuba wakati wa swala hiyo.

Sheikh ,Nasoro akiomba dua wakati wa swala hiyo.

Swala ikiendelea.
Swala ikifanyika.

Sheikh wa Mkoa wa Singida, Issa Nasoro (kushoto) akiwa na Katibu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Mkoa wa Singida wakiwa na mawakala wa uchinjaji wa wanyama wakielekea kukagua zoezi la uchinjaji eneo la Uhamaka lililopo Manispaa ya Singida.

Sheikh Nasoro na Katibu wa BAKWATA Mkoa wa Singida, Sheikh Burhan Mlau  (kushoto) wakizungumza na mmoja wa mawakala wa uchinjaji wanyama kutoka Uturuki.

Sheikh wa Mkoa wa Singida, Issa Nasoro akisalimiana na mmoja wa mawakala kutoka Uturuki.

Picha ya pamoja na mawakala wa uchinjaji wa wafanya hao.
Uchinjaji ukifanyika.
Kazi ya uchunaji ngozi wanyama hao ikifanyika.
 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad