SIMBACHAWENE ATEMBELEA BANDA LA MSD MAONESHO YA MAADHIMISHO WIKI YA UTUMISHI WA UMMA - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Wednesday, 19 June 2024

SIMBACHAWENE ATEMBELEA BANDA LA MSD MAONESHO YA MAADHIMISHO WIKI YA UTUMISHI WA UMMA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,George Simbachawene ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye Maonesho ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma ambayo yamefanyika kitaifa mkoani Dodoma akizungumza na viongozi wa Bohari ya Dawa (MSD) Kanda ya Kati wakati alipotembelea banda lao.

.................................

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

VIONGOZI mbalimbali wa Serikali wametembelea Banda la Bohari ya ya Dawa (MSD)  kwenye maonesho ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma ambayo yanafanyika  kitaifa mkoani Dodoma kuanzia tarehe 16 hadi 23 June, 2024.

Miongoni mwa viongozi waliotembelea ni Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo Mhe. George Simbachawene  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora pamoja na Mhe. Ridhiwani Kikwete (Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Mhe. Simbachawene amesema anafurahishwa na namna MSD inavyotekeleza majukumu yake katika kuhakikisha upatikanaji wa bidhaa za afya “nimefurahishwa na namna MSD ilivyosambaza mashuka kwenye majimbo yetu ambayo yamesaidia katika utoaji wa huduma za afya”

Mhe. Simbachawene ameipongeza pia MSD kwa kupeleka haraka Jokofu la kuhifadhia miili Kituo cha Afya Kibakwe – Mpwapwa - Dodoma ambalo lilikuwa linahitajika kwa kiasi kikubwa.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,George Simbachawene ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye Maonesho hayo akiwa katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa MSD alipo tembelea banda lao.
Wafanyakazi wa MSD wakifurahia jambo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,George Simbachawene ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye Maonesho.

 Picha ya pamoja.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad