.........................................
Na Dotto Mwaibale, Singidani Blog
Na Dotto Mwaibale, Singida
SHEIKH wa Mkoa wa Singida amemaliza kukagua vituo
vilivyotengwa kwa ajili ya zoezi la uchinjaji wa wanyama wakati wa Sikukuu ya Eid Al- Adha.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya
kukagua maeneo yote ya kuchinjia wanyama hao Sheikh Nasoro alizipongeza taasisi
zote zilizofanya vizuri kwa uchinjaji.
"Kuna baadhi ya taasisi zimefanya vizuri kwa
kufuata maelezo ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) na Serikali
kupitia idara ya mifugo ambapo zimechinja wanyama wenye sifa kama dini
inavyotaka, kutenga maeneo maalumu ya kuchinjia ambayo yamejengwa kisasa na
kuweka ulinzi wa kutosha kuepusha vurugu jambo ambalo kumekuwa na utulivu na
wananchi kupata sadaka yao bila ya bugudha," alisema Nasoro.
Sheikh Nasoro alizitaka taasisi ambazo
hazikufanya vizuri kuiga taasisi zilizofanya vizuri na kuwa jambo hilo ndio
hitaji la walaji wa wanyama hao wa sadaka.
Sheikh Nasoro alitoa wito kwa mawakala wa
wajichaji hao kujenga tabia ya kufuata maelekezo yanayotolewa na kununua
wanyama waliobora ambao wanalingana na thamani halisi ya hela wanazopewa na
wahusika kwa ajili ya kazi hiyo na si vinginevyo na kuacha tabia ya kununua
wanyama waliodhoofu kondefu na wagonjwa kwa bei ya chini lengo likiwa ni
kujipatia fedha na kuhatarisha afya za walaji wa nyama hiyo.
“Natoa
onyo kwa mawakala wote wanaokiuka taratibu na kanuni zilizowekwa kuacha tabia
ya kununu wanyama ambao hawana sifa ninawaomba wawe waadilifu vinginevyo hatuta
ruhusu wanyama wao kuchinjwa ,” alisema Sheikh Nasoro.








No comments:
Post a Comment