Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Singida (SUWASA) Hosea Magimbi akizungumzia Mradi wa Ujenzi wa Mabwawa ya kutibu Maji Taka Manga unaotekelezwa Kata ya Manga katika Manispaa ya Singida.
.........................
Na Dotto Mwaibale,
Singidani Blog
MAMLAKA ya Majisafi na
Usafi wa Mazingira Singida (SUWASA) imetoa vyeti vya kuwatambua wananchi wa
Kata ya Manga iliyopo Manispaa ya Singida ambao walitoa maeneo yao ya ardhi kwa
ajili ya kupisha utekelezaji wa Mradi wa Ujenzi wa Mabwawa ya kutibu majitaka Manga unaotekelezwa katika Manispaa hiyo.
Akizungumza
kwa niaba ya Mkurugenzi wa SUWASA katika hafla ya kukabidhi vyeti hivyo kwa
wananchi hao pamoja na kuelezea maendeleo ya mradi huo unaotekelezwa kwenye
eneo hilo Mkoa wa Singida, Hosea Magimbi alisema mradi huo ni wa muhimu sana.
Alisema
mradi huo umegharimu zaidi ya Sh. Bilioni 1.7 fedha ambazo zimetolewa na
Serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya
Chama Cha Mapinduzi (CCM) eneo la Kata ya Manga kupitia mkandarasi ambaye
atakuwa chini ya usimamizi wa SUWASA.
Magimbi alisema mradi huo ni wa karne kwa maana kwamba mji wa Singida haujawahi
kupata mradi wa aina hiyo hivyo mradi huo ni wa kwanza na wananchi waliowengi
wanahitaji kunufaika nao.
“Mradi huu
utawanufaisha wananchi wengi kwa kuwaondolea adha ya maji taka kutoka kwenye
majumba yao na kuyapeleka katika mabwawa hao yatakayojengwa eneo hilo na kutibu
maji taka,” alisema Magimbi.
Magimbi
alitumia nafasi hiyo kuwashukuru wananchi wa eneo hilo kwa kuwapa ardhi kupisha
mradi huo na katika kuthamini mchango wao huo wamewatunuku vyeti maalumu ili
iwe kumbukumbu kwao na SUWASA.
Aidha,
Magimbi aliwaomba wananchi wa eneo hilo waendelee kutoa ushirikiano wakati wote
wa utekelezaji wa mradi huo hadi hapo utakapo kamilika.
Diwani wa
Kata ya Manga, Ramadhan Yusuph alisema mradi huo ni wa muhimu kwa wananchi wa
eneo hilo kwani watayatumia maji hayo ambayo yatasafishwa kitaalamu kwa ajili
ya kuanzisha kilimo cha mboga mboga hivyo uchumi wa wana Manga utakuwa kupitia
uuzaji wa bidhaa zitakazotokana na kilimo hicho.
Mkazi wa
Kata hiyo Juma Chima alisema walikuwa na changamoto kubwa ya maji hasa wakati
wa kiangazi hivyo anawashuru SUWASA kwa kuwapekea mradi huo ambao una kwenda
kuwa mkombozi kwao
Abubakari
Misughaa mazi wa kijiji hicho alianza kuishukuru Serikali kupitia SUWASA kwa
kuwapelekea mradi huo na kueleza kuwa SUWASA wamefika wakati muafaka ndani ya
kijiji hicho kuwapelekea mradi huo ambao utakuwa na manufaa makubwa kwa
wananachi ambao watakuwa wakiishi kandokando ya mabwawa hayo.
Alisema
baadhi ya faida watakayoipata wananchi hao ni kuanzisha kilimo cha umwagiliaji
na mbogamboga kilimo ambacho kitabadilisha maisha yao kwa kuinuka kiuchumi na
kueleza kuwa SUWASA kwao imekuwa na faida kubwa kwani wamewapelekea maji ya
kutumia wananchi na kusambazwa katika taasisi zote za Serikali.


















No comments:
Post a Comment