Vijana wa Kata ya Itigi wakifurahia jambo wakati wa kikao kazi kilichofanyika Juni 19, 2024 mkoani Singida
......................
Na Dotto Mwaibale
VIJANA wa Kata ya Itigi mjini mkoani
Singida wametakiwa kufanya kazi kwa bidii na kuzitumia vizuri fursa zilizopo
wilayani humo kwa lengo la kujikomboa kiuchumi hasa katika kufanya kilimo na
biashara
Ombi hilo limetolewa na Diwani wa Kata
hiyo 𝐴𝑙𝑙𝑦 𝑀𝑖𝑛𝑗𝑎 wakati akizungumza na vijana hao katika kikao kazi kilichowakutanisha
na wadau mbalimbali kilicho keti Juni 19, 2024 kwa lengo la kuzungumzia
fursa zilizopo kwenye kata hiyo.
"Vijana mna kila sababu ya
kuzichangamkia fursa zilizopo kwenye kata yetu hasa ya kilimo na biashara badala ya kukaa tu mkipoteza
muda," alisema Minja.
Pamoja na mambo mengine katika kikao
hicho viongozi wa kata hiyo waliweza kutoa elimu kwa vijana hao waliweza
kupatiwa elimu ya ujasiriamali na athari za dawa za kulevya kwa kundi hilo.
Kwa upande wake Afisa 𝑀𝑡𝑒𝑛𝑑𝑎𝑗𝑖 wa 𝑘𝑎𝑡𝑎 hiyo, 𝑆𝑎𝑖𝑚𝑜𝑛 𝑆𝑖𝑟𝑖𝑙𝑜, 𝑎𝑙𝑖𝑡𝑜𝑎 𝑒𝑙𝑖𝑚𝑢 𝑦𝑎 𝑢𝑗𝑎𝑠𝑖𝑟𝑖𝑎𝑚ali na kuwasisitiza vijana hao 𝑘𝑢𝑎𝑐ℎ𝑎𝑛𝑎 𝑛𝑎 𝑚𝑎𝑚𝑏𝑜 𝑦𝑎𝑠𝑖𝑦𝑜 𝑛𝑎 𝑡𝑖𝑗𝑎 𝑏𝑎𝑑𝑎𝑙𝑎 𝑦𝑎𝑘𝑒 wafanye kazi kwa bidii ili kuiletea maendeleo kata hiyo.
Naye 𝑃𝑎𝑠𝑐ℎ𝑎𝑙 𝑀𝑎𝑠𝑠𝑒𝑙𝑒, alizungumzia 𝑗𝑢𝑢 𝑦𝑎 𝑎𝑡ℎ𝑎𝑟𝑖 𝑧𝑎 𝑑𝑎𝑤𝑎 z𝑎 𝑘𝑢𝑙𝑒𝑣𝑦𝑎 𝑛𝑎 𝑗𝑖𝑛𝑠𝑖 zitakavyoweza kukatisha ndoto zao za maisha na kujikuta wakishindwa
kuinuka kimaisha na kuinua uchumi wa Taifa baada ya kupoteza nguvu kazi.
Afisa 𝑀𝑡𝑒𝑛𝑑𝑎𝑗𝑖 wa 𝑘𝑎𝑡𝑎 hiyo, 𝑆𝑎𝑖𝑚𝑜𝑛 𝑆𝑖𝑟𝑖𝑙𝑜 akitoa mada kwenye kikao hicho.










No comments:
Post a Comment