HIFADHI YA MIKUMI WAKABIDHI MADAWATI 213 KWA SHULE ZA MSINGI SABA KILOSA. - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Thursday, 20 June 2024

HIFADHI YA MIKUMI WAKABIDHI MADAWATI 213 KWA SHULE ZA MSINGI SABA KILOSA.

Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Shaka Hamdu Shaka (kushoto) akikabidhiwa madawati 213 na Afisa Mwandamizi wa Uhifadhi Buka Alfred yenye thamani zaidi ya Sh. milioni 18.

Na Mwandishi Wetu, Morogoro

Katika kuendelea Kuunga mkono juhudu za serikali kwenye sekta ya elimu Hifadhi ya Taifa Mikumi  imetoa msaada wa Madawati Kwenye Shule za msingi saba zinazozunguka hifadhi hiyo kwenye kata za Mhenda,Ruhembe na Mikumi.

Akizungunza katika hafla ya kukabidhi madawati kaimu Mhifadhi Mkuu Hifadhi ya Taifa Mikumi. Afisa mwandamizi wa uhifadhi Buka Alfred amesema wametoa madawati 213 yenye Thamani zaidi ya Sh. milioni 18.

Buka anasema Hifadhi hiyo  imekua na utaratibu wa kurejesha Kwa Wananchi Ili  jamiii iwe  mabalozi wa masuala ya uhifadhi hasa watoto wadogo.

Anasema kumekua na tabia baadhi ya vijiji vinayozunguka Hifadhi kufanya shughuli sio rasmi kwenye Hifadhi ikiwemo uwindaji haramu ,ufugaji , kilimo na kuchoma moto jambo ambalo limekua Changamoto hivyo utolewaji wa Madawati hayo ni Kuona matunda ya  uhifadhi.

Naye Mkuu wa Kitengo cha ujirani mwema Hifadhi ya Taifa Mikumi Afisa daraja la kwanza Uhifadhi Hamisi Marwa amezitaja shule hizo kuwa ni shule ya  Kitete msindazi ,Mikumi,Mikumi town,Mikumi mpya ,Mhenda,Kielezo na Ruhembe .

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Shaka Hamdu Shaka amesema wilaya hiyo ina uhaba wa madawati elfu kumi na sita kwa sasa serikali inaendelea na kutatua changamoto hiyo ambapo tayari madawati elfu nane yamepatikana na Hadi ifikapo disemba mwaka huu changamoto hiyo itamalizika.

Shaka amesema  serikali inatambua mchango wa wadau mbalimbali  katika sekta ya elimu na itaendelea kushirikiana kuinua taaluma

Amesema Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Dokta Samia Suluhu Hassan  ametoa bil.1.8 kwa Ajili ya ujenzi wa madarasa , matundu ya vyoo pamoja na Madawati yake hivyo fedha hizo zitaelekelzwa kukabiliana na Changamoto ya uhaba wa madawati.

Makabidhiano ya madawati hayo yakifanyika.
Muonekano wa madawati hayo.

 Kazi ya kupokea madawati hayo ikiendelea

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad