VIJIJI VYOTE MKOA WA SINGIDA VIMEFIKISHIWA UMEME - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Thursday, 6 June 2024

VIJIJI VYOTE MKOA WA SINGIDA VIMEFIKISHIWA UMEME

Naibu Waziri wa Nishati,  Judith Kapinga (kushoto), ambaye alikuwa mgeni rasmi akikata utepe kuashiria uwashaji wa umeme katika vijiji viwili vya Mwasauya na Mdilu vilivyopo Wilaya ya Singida katika hafla iliyofanyika June 5, 2024. Kutoka kulia aliyeshika Maiki .ni Afisa Uhusiano na Huduma kwa Wateja TANESCO Mkoa wa Singida, Rehema Mwaipopo, Diwani wa Kata ya Mwasauya, Salum Juma na Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini Ramadhan Ighondo.

...........................

Na Dotto Mwaibale, Singidani Blog.

NAIBU Waziri wa Nishati,  Judith Kapinga amesema kutokana na uchapakazi mzuri wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan vijiji vyote vya Mkoa wa Singida tayari vimefikishiwa umeme huku vijiji 84 vya Singida Kaskazini vikinufaika kasoro vinne ambayo navyo vitapata kabla ya June 15, 2024 kwani wakandarasi wapo kazini.

Kapinga ambaye alikuwa mgeni rasmi alitoa kauli hiyo June 5, 2024 wakati wa hafla ya uwashaji wa umeme katika vijiji viwili vya Mwasauya na Mdilu vilivyopo Wilaya ya Singida kupitia Mradi wa Wakala wa Nishati Vijiji (REA) Awamu ya Tatu, mzunguko wa pili kwa kushirikiana na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO)

“Kazi hii kubwa aliyoifanya Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan napenda kusema mnyonge mnyongeni lakini haki yake wacha apewe,” alisema Kapinga huku akishangiliwa.

Kapinga alisema maendeleo ni hatua na kuwa ilikuwa ni lazima umeme uvikishwe kwanza kwenye vijiji ndipo upelekwe katika  vitongoji vyote na hiyo ndiyo dhamira ya Serikali.

Alisema katika mwaka huu wa fedha wa 2024/ 2025 Serikali imetenga fedha kwa ajili ya kufikisha umeme katika vijiji 4000 kazi ambayo itafanywa kwa awamu.

Aidha, Kapinga alisema miradi ya umeme ya namna hiyo inatekelezwa katika kila kijiji hapa nchini ambapo kwa Mkoa wa Singida zaidi ya Sh. Bilioni 80 zimetumika kwa kazi hiyo ambapo alitumia nafasi hiyo kuwaomba wanananchi kuendelea kuunga mkono jitihada anazozifanya Rais Samia na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini, Ramadhan Ighondo  akizunghumza kwenye hafla hiyo alimuomba Naibu Waziri wa Nishati Judith Kapinga kuviongezea umeme vijiji uwe na nguvu ili wananchi wake waweze kufungua viwanda ambavyo vitainua uchumi wao baada ya kuanzisha viwanda vya kuzalisha bidhaa za aina mbalimbali.

Kwa upande wake Meneja wa TANESCO Kanda ya Kati, Mhandisi DanstanNdamugoba alisema shirika hilo linaendelea kutoa huduma kwa wananchi na kuwa Mkoa wa Singida una jumla ya vijiji 441 na mpaka sasa vijiji 437 vimewashwa umeme na vilivyobaki ni vijiji vinne tu na ifikapo June 15, 2024 vijiji vyote vitakuwa vinawaka umeme.

Naye Meneja wa Usimamizi wa Miradi Wakala wa Nishati Vijijini (REA) ambaye alimwakilisha Mkurugenzi Mkuu REA, Mhandisi Romanus Lwena alisema Wilaya ya Singida ina jumla ya vijiji 84 ambavyo vimefikishiwa umeme kasoro vinne na kuwa vitongoji vipo 439 kati ya hivyo vitongoji 275 tayari vimefikishwa umeme na ambavyobado ni 164.

“Nitoe wito kwa wananchi wa vijiji hivyo kuwaeleza kwamba Serikali imetoa fedha nyingi kwa ajili ya kutekeleza miradi hiyo akitolea kwa Wilaya ya Singida peke yake imetoa Sh.Bilioni 10 na kwa mkoa wote wa Singida ni zaidi ya Sh. Bilioni 86 hivyo kwa yale maeneo ambayo tayari umeme wamepata tunawaomba wananchi wajitokeze kuutumia kwa kuwekeza miradi mbalimbali ya kiuchumi ili lengo la Serikali litimie,” alisema Mhandisi Lwena.

Baadhi ya wananchi wa vijiji hivyo wakizungumza kwa nyakati tofauti walimshuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwakamilishia mradi huo kupitia REA na Tanesco na kuwa sasa wanakwenda kubadilika kiuchumi kutokana na matumizi sahihi ya nishati hiyo.

Naibu Waziri wa Nishati,  Judith Kapinga, ambaye alikuwa mgeni rasmi akizungumza na wananchi (hawapo pichani) wakati wa hafla ya uwashaji wa umeme katika vijiji viwili vya Mwasauya na Mdilu vilivyopo Wilaya ya Singida 
Naibu Waziri wa Nishati,  Judith Kapinga na viongozi wengine wakipunga mkono wakati walipokuwa wakiwasili kwenye hafla hiyo Kijiji cha Mwasauya. 
Naibu Waziri wa Nishati,  Judith Kapinga, ambaye alikuwa mgeni rasmi akifurahi na wananchi wa Kata wa Mwasauya wakati wa hafla hiyo. 

Furaha ikitamalaki Kijiji cha Mdilu wakati wa hafla ya uwashaji wa umeme kijini hapo.

Meneja wa Usimamizi wa Miradi Wakala wa Nishati Vijijini (REA) ambaye alimwakilisha Mkurugenzi Mkuu REA, Mhandisi Romanus Lwena akizungumzia mradi huo.

Meneja wa TANESCO Kanda ya Kati, Mhandisi DanstanNdamugoba akizungumza na waandishi wa habari kuhusu faida ya mradi huo.
Mkuu wa Wilaya ya Singida, Godwin Gondwe akiteta jambo na Meneja wa Tanesco Mkoa wa Singida, Mwamvita Ally wakati wa hafla hiyo.
Kikundi cha Ngoma ya Asili cha Kabila la Wanyaturu kikiimba wito wenye maudhui ya ukaribisho wa kumkaribisha Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga.
Diwani wa Kata ya Mwasauya Salum Juma akiwasalimia wananchi wakati wa hafla hiyo iliyofanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi, Mdilu.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Mdilu, Samson Samuel akizungumza.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Wilaya ya Singida, Shabani Mang'ola akizungumzia faida ya mradi huo ambapo alisema moja ya faida ya umeme ni kuzungumza kiingereza bila ya kutegemea.
Mkazi wa Kijiji cha Mwasauya Halima Said akiweka radio zake juani ili zijichadi na aweze kuzitumia lakini hivi sasa ataachana na adha hiyo baada ya umeme kuwashwa rasmi katika kijiji hicho.
Miundombinu ya Tanesco ikionekana katika Kata ya Mwasauya baada ya kufungwa.

Watoto wa Kata ya Mwasauya wakishiriki hafla hiyo.



Hafla ikiendelea.
Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini akiwasalimia wananchi katika mkutano wa hadhara wakati wa hafla hiyo.
Wananchi wa Kata ya Mwasauya wakiserebuka kufuarahia uwashaji wa umeme.
Taswira ya hafla hiyo.
Afisa Tarafa wa Ilongero, Yahaya Njiku akizungumza wakati akiongoza itifaki wakati wa hafla hiyo.

 ---ANGALIA VIDEO CHINI---

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad