CHAMA SOKA LA WANAWAKE MKOA WA TABORA (TAWFA) WACHAGUANA - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Friday, July 12, 2024

CHAMA SOKA LA WANAWAKE MKOA WA TABORA (TAWFA) WACHAGUANA

Katibu wa soka la wanawake Mkoa wa Tabora Blandina Michael 

...................................

 Na Hastin Liumba,Tabora 

CHAMA cha soka la wanawake mkoa wa Tabora (TAWFA) wamefanya uchaguzi wa viongozi wao ambao watadumu kwa muda wa miaka minne kwa mujibu wa sheria za soka duniani. 

Akiongea na waandishi wa habari mwenyekiti wa cha hicho cha TAWFA) Farida Nydamkama alisema uchaguzi ulifuata taratibu zote zinazoelekekwa na TFF. 

Mwenyekiti Farida alisema wajumbe waliopiga kura walikuwa ni wajumbe saba ambao kwa kuwataja ni timu za The kick Queens,Mpera Queens,Veta Queens,Ziba Queens,Manonga Queens,Es Unyanyembe Queens na Unyanyembe Queens. 

Aidha alisema katika nafasi aliyopata katika soka la wanawake ana mikakati ya kuimarisha miundombinu ya soka la wanawake ili watoto wa kike wacheche mpira katika viwanja vilivyo boya bora kwa kujibu wa maagizo ya TFF na FIFA. 

Alisema jambo lingine kama mwenyekiti ni kuhamasisha na kuendeleza watoto wa kike waweze kucheza mpira wa miguu kama ilivyo duniani kote. 

Aidha aliongeza kuwa eneo jingine katika uongozi wake ni kuimarisha na kuendelea mpira wa miguu kwa watoto wa kike wapende wacheze mpira huo ndani na nje ya nchi. 

Kwa upande wake Katibu wa soka la wanawake Mkoa wa Tabora Blandina Michael alisema kama mtendaji wa chama kazi ya mbele yake ni utafutaji wa ufadhili.

Michael anaongeza kuwa kazi yake kama mtendaji wa chama ni kuhamasisha wazazi na walezi waupende mpira wa miguu wa soka la wanawake kwa sababu ni ajira na uchumi.

Aisha alisisitiza na kuhamasiasha kama chama kupitia vyombo vya habari ni kukuza na kutengeneza ukaribu wa kimkakati ili kuutangaza mkoa wa Tabora na fursa zilizopo. 

Hata hivyo aliongeza kuwa mipango yake mingine kama katibu wa chama hicho ni kuanzisha bonanza ambayo itaambata na michezo mbalimbali ikiwemo upimaji VVU na utoaji damu salama. 

Aidha alisema pia katika hayo pia kutakuwa na kufanya usafi katika sehemu au taasisi za serikali  kama hosptali ya rufaa Kitete na maeneo mengine ambayo ni sehemu ya serikali.

 Alitoa wito kwa wizara inayohusika kuwaunga mkono mipango ya chama cha soka la wanawake mkoa wa Tabora kwani wana mipango mizuri lakini hawana ufadhili hivyo wanamuomba mkuu wa mkoa wa Tabora Poul Matiko Chacha kuliona hilo. 

Michael alimalizia kwa kuwaomba wanasiasa wa mkoa wa Tabora nao kutumia nafasi ya soka la wanawake kuwatangaza wao kwa kazi nzuri wanayoifanya ili sasa kama soka wanawake ili hata Rais Dkt Samia Suluhu Hassan (SSH) asikie kilio chetu. 

Aidha aliwataja uongozi wa chama hicho kwa sasa ni Farida Ndyankama mwenyekiti,Caherine Bundala makamu mwenyekiti,Taus Changaluma mjumbe,Tulakia Kiwele mjumbe Upendo Mgalula mjumbe,Blandina Michael katibu wa chama na Anna Mwingira mjumbe mkutano mkuu wa chama soka la wanawake.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad