DC MBINGA AZINDUA MATUMIZI YA NISHATI MBADALA YA MAKAA YA MAWE - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Friday, July 12, 2024

DC MBINGA AZINDUA MATUMIZI YA NISHATI MBADALA YA MAKAA YA MAWE

  ·Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Kisare Makori, akiongoza hafla ya  uzinduzi wa matumizi ya nishati safi na salama inayotokana na makaa ya mawe iliyoandaliwa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma.

.........................

Na Mwandidhi Wetu, Mbinga

MKUU wa Wilaya ya Mbinga Kisare Makori amezindua matumizi ya nishati safi na salama InaYotokana na makaa ya mawe kwa ajili ya matumizi katika shule za msingi na sekondari za Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma.

Hafla hiyo ya uzinduzi iliyoandaliwa na Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga imefanyika katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya Wasichana Mbinga iliyoko Kata ya Kingonsera.

Hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, v kisiasa akiwemo Katibu wa CCM Wilaya ndugu Madodi, viongozi wa dini akiwemo Askofu wa Jimbo Kuu la  Mbinga, John Ndimbo na Sheikh wa wilaya,, sekta binfsi na makampuni yanayochimba makaa ya mawe.

Awali akitoa taarifa ya mkakati wa halmashauri katika utekelezaji wa maelekezo ya serikali kuhusu matumizi ya nishati safi kwenye maeneo yanayotoa huduma ya chakula kwa zaidi ya watu 100, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga, Joseph Kasusura ameeleza kuwa lengo la halmashauri ni kuhakikisha kuwa shule zote za msingi na sekondari katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga zinatumia nishati mbadala iliyo safi na salama.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Kisare Makori alisema "Suala la matumizi ya nishati safi ni jukumu la kila mmoja katika ngazi za familia, taasisi na hata katika vikundi mbalimbali"

Makori alisema changamoto za matumizi ya nishati chafu na isiyo salama imekuwa ikionekana wazi katika nyanja mbalimbali za kijamii, kiuchumi, kiafya na kimazingira ikiwemo ongezeko la ukataji miti ovyo.

Alisema vitendo hivyo vinachangia katika mabadiliko ya tabia nchi, kupotea kwa mimea na viumbe hai pamoja na kusababisha athari za kiafya kwa wananchi hasa wanawake wanaotumia nishati hiyo kupikia.

Makori ametumia fursa hiyo kuipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga kwa kuwa mfano mzuri wa kuhakikisha Mbinga inaandika  historia ya kuanza safari ya kuachana na matumizi ya kuni, mkaa na nishati nyingine isiyofaa katika shule.

·Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Kisare Makori, akihutubia wakati wa uzinduzi huo.
Uzinduzi ukifanyika.
Hafla ikiendelea.
Viongozi wakiwa meza kuu.
·Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Kisare Makori, akiteta jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga, Joseph Kasusura wakati wa uzinduzi huo.

 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga, Joseph Kasusura, akizungumza kwenye hafla hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad