MSD YACHANJA MBUGA YABORESHA UTENDAJI KAZI - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Thursday, July 4, 2024

MSD YACHANJA MBUGA YABORESHA UTENDAJI KAZI

Mkurugenzi Mkuu wa  Bohari ya Dawa (MSD), Bw. Mavere TukaI, akizungumza na Wahariri wa vyombo vya habari (hawapo pichani waliotembelea MSD Kanda ya Kati kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na taasisi hiyo.

......................................

Na Dotto Mwaibale, Dodoma

BOHARI ya Dawa (MSD) imeendelea kuchanja mbuga baada ya kufanya maboresho makubwa ya utendaji kazi wake na kuhakikisha bidhaa za afya zinafika kwa wateja wao kwa wakati.

Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Mavere Tukai akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari ambao walikuwa katika ziara ya kutembelea na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na MSD Kanda ya Dodoma na Kanda ya Iringa ambapo walipata fursa ya kufika Kiwanda cha kuzalisha mipira ya mikono (Groves) cha Idofi kilichopo Makambako Mkoa wa Njombe alisema wamefanya maboresho makubwa ambayo wanajivunia.

"Kama mnavyoweza kukumbuka miaka michache iliyopita huduma zetu tulizokuwa tukizitoa zilikuwa chini ya asilimia  50 lakini tuliendeea kupambana hadi kufikia mwaka 2022/ 2023 tuliweza kufikia asilimia 71 na tulipofanyiwa ukaguzi tulikuwa tumefika asilimia 76," alisema Tukai.

Alisema mwaka huu hadi kufikia robo ya tatu ya mwaka walikuwa wamefikia asilimia 84    jambo ambalo kwao limekuwa la mafanikio na kueleza kwamba licha ya kazi hiyo nzuri wanayoifanya lakini bado hawajatimiza malengo yao ya kufika asilimia 90.

Tukai alisema kazi nyingine  kubwa waliyoifanya ni kufanya maboresho ya utendaji kazi kwa kuuacha ule wa zamani na kujikita zaidi kidijitali ambapo wamelazimika kuacha kutumia karatasi.

Alisema kupitia mfumo huo unaoonesha muda mtumishi aliofika kazini, muda aliofanya kazi na pia unamtathimini mtu muda alioingia na kutoka kazini na kuwa umesaidia kuchochochea utendaji wa kazi na kwamba wauunda  kwa kushirikiana na washauri elekezi .

Alisema maboresho mengine waliyofanya ni kuongeza magari, ujenzi wa maghara makubwa ya kisasa katika baadhi ya mikoa ili kurahisisha ufikishaji wa bidhaa hizo za afya kwa walengwa.

Mwanahabari Mgaya Kingoba akizungumza katika kikao hicho cha mafanikio ya MSD katika utendaji wake.

Mwanahabari Bakar Kimwanga akizungumza kwa niaba ya waandishi wenzake.

Mwanahabari John Bukuku akiuliza swali.

Mwanahabari Stella Aron akizungumzia kuhusu ziara hiyo.
Mwanahabari Taus Mboya akizungumzia ziara hiyo.



Mkutano na waandishi wa habari ukiendelea.
Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad