SHIRIKA LA KICKSTART LATOA PAMPU ZA UMWAGILIAJI KWA WAKULIMA SINGIDA - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Thursday, July 4, 2024

SHIRIKA LA KICKSTART LATOA PAMPU ZA UMWAGILIAJI KWA WAKULIMA SINGIDA


Mkuu wa Wilaya ya Singida,Godwin Gondwe akipokelewa na Meneja Mkazi wa Shirika lisilo la Kiserikali la Kimataifa la KickStart  International alipowasili ya kuzindua na kukabidhi pampu za Umwagiliaji za MoneyMaker kwa wakulima wadogo iliyofanyika Kijiji cha Mtipa Manispaa ya Singida, Julai 3, 2024 

.......................................

Na Dotto Mwaibale, Singida

SHIRIKA lisilo la Kiserikali la Kimataifa la KickStart  International  ambalo limesajiliwa nchini Marekani  lenye makao makuu yake jijini Dar es Salaam limeyakutanisha mashirika mengine ya MEDA, Kampuni ya TAISH na SEMA ya Mkoa wa Singida kwa lengo la kushirikiana kuwasaidia wanawake katika ufanyaji wa kilimo cha umwagiliaji kwa kutumia pampu zinazotolewa na shirika hilo za MoneyMaker.

Meneja Mkazi wa shirika hilo Mwaluko Mpangwa akizungumza na waandishi wa habari Julai 3, 2024 Kijiji cha Mtipa kilichopo Manispaa ya Singida wakati wa hafla ya kuzindua na kukabidhi pampu za Umwagiliaji za MoneyMaker alisema kilimo hicho na kutumia pampu hizo ni cha muhimu sana kwani hakisubiri mpaka mvua iwepo.

Mpangwa alisema dhima ya shirika hilo ni kuwainua wakulima wadogo kupitia kilimo cha umwagiliaji ambapo wanataka walau kila kaya iwe na eneo ambalo linamwagiliwa maji kwa mwaka mzima ili mvua zikikoma kunyesha waendelee na kilimo bila ya kusubiri mvua.

“Vyanzo vya maji kama visima, mabwawa, maziwa na mito tunavyo hivyo tunawahimiza wakulima wafanye kilimo cha umwagiliaji kama tunavyo jua kuwa hivi sasa dunia inapita katika changamoto ya tabia nchi na waathirika wakubwa ni nchi 17 ziliopo zilizopo jangwa la Sahara na Tanzania ikiwepo,” alisema Mpangwa.

Mkuu wa Wilaya ya Singida,Godwin Gondwe akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Singida alilishukuru shirika hilo kwa kwenda kuendesha mradi huo mkoani Singida.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika Sustainable Environment Management Action - SEMA

ambalo limeingia ubia wa ushirikiano na shirika hilo,  Ivo Manyaku alisema mradi huo umejikita katika maeneo makubwa mawili moja kupitia Kampuni ya Taish Farm ambao wanashughulika upande wa mifugo kuhakikisha ni namna gani watawasaidia wanawake ambao wanafuga mifugo katika kiwango cha chini na kuweza kuboresha kupata  maziwa ambayo yatanunuliwa na kampuni hiyo.

“Sisi Sema kutokana na kufanya kazi Mkoa wa Singida tunawakulima wengi ambao tunefanya nao kazi na kufanya nao mawasiliano nao waliopo mbali na Singida na kuweza kuwaunganisha na kampuni ya Taish, MEDA na shirika la  KickStart  kupata mahitaji ambayo watayahitaji ili kuweza boresha maisha yao kutokana na shughuli za kilimo na ufugaji kwa kutumia kilimo cha umwagiliaji. 

Naye Mkurugenzi wa Kampuni ya TAISH Farm, Hassan Rajabu alisema ushiriano uliopo baina ya mashirika hayo umekuwa na tija kubwa katika uboreshaji wa shughuli zao za kuwainua wakulima kiuchumi. 

Mratibu wa mradi kutoka shirika la MEDA, Rebeka Rugola alisema shirika hilo linafanya kazi na washirika wao kwa ajili ya kujenga mazingira wezeshi kwa makundi ya wanawake na wajasiriamali. 

Mkulima mdogo wa mbogamboga, Victor Elias mkazi wa Mwankoko Manispaa ya Singida akizungumza kwa niaba ya wenzake  baada ya kupewa Pampu ya Umwagiliaji ya MneyMaker alilishukuru shirika hilo na kueleza kwamba sasa ataachana uchotaji wa maji kwa kutumia ndoo na badala yake atatumia pampu hiyo aliyopewa na shirika hilo na kuongeza mazao. 

Meneja Mkazi wa shirika hilo Mwaluko Mpangwa akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Meneja Mkazi wa shirika hilo Mwaluko Mpangwa akizungumza na wanawake wajasiriamali wakati wa hafla hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Singida, Godwin Gondwe akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa ambaye alikuwa mgeni rasmi.
 Mkurugenzi wa Kampuni ya TAISH Farm, Hassan Rajabu akizungumza.
Mkuu wa Wilaya ya Singida, Godwin Gondwe akijaribu kutumia moja ya pampu hizo za umwagiliaji.
Uzinduzi wa pampu hiyo ukifanyika.
Uzinduzi ukiendelea kufanyika.
Pampu zikikabidhiwa kwa wakulima.
 Muonekano wa pampu hizo kabla ya kukabidhiwa walengwa.
(PICHA ZOTE NA SOLOMON PHILEMON)

---ANGALIA VIDEO CHINI--

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad