Ongezeko la Safari litahusisha kuanza kwa treni mpya ya haraka (Express
train) ambayo itakuwa ikifanya safari kati ya Dar es Salaam na Morogoro bila
kusimama vituo vya kati.
Mabadiliko ya ratiba yatakuwa kama ifuatavyo; Treni ya haraka itakuwa
ikiondoka Dar es Salaam saa 12:00 asubuhi na saa 1:10 usiku. Treni itaondoka
Morogoro saa 12:20 asubuhi na saa 1:30 usiku.
Treni ya kawaida itakuwa ikiondoka Dar es Salaam saa 3:30 asubuhi na saa
10:00 jioni na itaondoka Morogoro saa 3:50 asubuhi na saa 10:20 jioni.
Abiria anashauriwa kukata tiketi kupitia njia ya mtandao au madirisha ya
tiketi yaliyo ndani ya vituo vya treni saa 2 kabla ya muda wa safari ili
kuepuka msongamano.
Shirika litaendelea kuongeza idadi ya safari kulingana na ongezeko la idadi ya abiria ili kutoa huduma bora na za uhakika.
Jamila Mbarouk
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano








No comments:
Post a Comment