Na Kulwa Mwaibale, Dar es Salaam
WALIOKUWA Wafanyakazi wa Mamlaka ya Usalama wa Usafiri wa Anga Tanzania, wameanzisha umoja wao ambao kwa kifupi unaitwa (USAWA)
Akizungumza mwishoni mwa wiki wakati wa hafla ya kupitisha Katiba ya umoja huo iliyojiri Mikwambe, Kigamboni, Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Umoja huo, Margareth Kyarwenda, alisema lengo la kuanzisha umoja huo ni kusaidiana wakati wa shida na raha.
Aliongeza kuwa, wazo la kuanzisha umoja huo walilipata mwaka 2021 baada ya kuona manufaa ya kushirikiana katika shida na raha, na hivyo kuwafikishia wazo hilo wengine ambalo walilipokea kwa mikono miwili," alisema Kyarwenda.
Aliongeza kuwa Mwaka huohuo 2021 wakachagua viongozi wa mpito, ambao Mwenyekiti akawa yeye, Makamu Mwenyekiti akawa Aspedito Mfugale, Katibu Juda Mkai, Katibu msaidizi Aurelia Mushi na Mtunza Hazina akawa Lawrence Paul.
Kyarendwa alisema ilipotokea mmoja wao anaumwa, kufiwa, sherehe kama vile harusi, waliendelea kusaidiana.
Wakiendelea na utaratibu huo, wakaamua kuwa na Umoja ulio rasmi,na hivyo kuandaa Katiba ambayo ilipitishwa Julai 6,2024 baada ya kumalizika kwa mchakato wake.
"Leo Julai 6 ndiyo tumekutana tena hapa katika mkutano huu wa nne kwa lengo la kupitisha katiba yetu,namshukuru Mwenyezi Mungu wana USAWA wapatao 32 wameshiriki na ni imani yetu hatua itakayofuata itakuwa na mafanikio makubwa," alisema mwenyekiti huyo.
Kyarwenda ambaye kwa mjibu wa Katiba, alichaguliwa kuwa Mwenyekiti rasmi kwa miaka miwili ijayo, amesema kuwa,umoja wao una hazina kubwa ya wataalam mbalimbali, kwa kutumia uzoefu walionao ambapo baadhi yao wameupata nje ya nchi, wako tayari kutoa ushauri kwa maswala yahusuyo Usalama wa Usafiri wa Anga wakati wowote watakapohitajika.
Katibu wa USAWA wa sasa, Aurelia Mushi, akizungumza wakati wa hafla hiyo, aliwapongeza waliotoa wazo la kuanzishwa kwa umoja huo ambao wamesema umewaunganisha tena baada ya kustaafu, na kuwaleta pamoja.
"Bila umoja huu huenda ingekuwa vigumu kuonana na wastaafu wenzetu kama ndugu yangu Ulimboka Mwakilili anayeishi huko Mbeya na Kaka Simon Kimiti yule pale anayeishi Arusha," alisema katibu huyo.
Mwakilili alitoa rai kwa wastaafu wenzake kudumisha upendo, mshikamano, kujitoa kwa hali na mali,jambo litakaloufikisha mbali umoja wao utakaorithiwa na wote watakaofanya kazi katika mamlaka hiyo ya Usalama wa Usafiri wa Anga nchini.
Aliongeza kuwa, siku za usoni watabuni miradi kwa ajili ya umoja huo ili kupata kipato kitakachoinua uchumi wao na taifa kwa ujumla.
Wakati wa hafla hiyo, iliyohudhuriwa na wastaafu kutoka baadhi ya Mikoa, ulifanyika uchaguzi uliowaweka Madarakani viongozi wapya akiwemo pia Mweka Hazina Mteule Said Ulaya.
Katika tukio hilo la kihistoria, wastaafu watano wenye umri wa miaka 75 na
zaidi, ambao ni Steve Mworia,Saltieli Munisi,Lawrence Paul,Aggrey Maeda,Fred
Kitangwa, walitunukiwa tuzo mbalimbali







No comments:
Post a Comment