SHEIKH MKOA WA SINGIDA AWATAKA VIJANA KUMRUDIA MUNGU - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Sunday, July 7, 2024

SHEIKH MKOA WA SINGIDA AWATAKA VIJANA KUMRUDIA MUNGU

 Sheikh wa Mkoa wa Singida, Issa Nasoro akizungumza wakati wa Swala ya Ijumaa iliyofanyika Julai 4, 2024

 Sheikh wa Msikiti wa Masjid Noor uliopo Kata ya Misuna Manispaa ya Singida, Omar Is-Haka akizungumza wakati wa Swala ya Ijumaa iliyofanyika Julai 4, 2024.

...................

Na Dotto Mwaibale

SHEIKH Mkoa wa Singida, Issa Nasoro amewataka vijana kurejea kwa Mungu na kutoshawishiwa na wanasiasa ili kuharibu amani ya nchi tuliyoachiwa na waasisi wa Taifa la Tanzania.

Akizungumza na Waumini wa dini ya Kiislamu katika swala ya Ijumaa iliyofanyika Julai 4, 2024 Msikiti wa Masjid Noor uliopo Kata ya Misuna Manispaa ya Singida aliwataka vijana hao kutoshawishina na baadhi ya wanasiasa ambao hawaitakii mema nchi yetu.

“Vijana msidanganyike na wanasiasa hao simameni kwenye misingi ya dini bila kuyumbishwa kwani wanataka kuwatumieni hivyo nawaomba ujana wenu utumieni vizuri na si vinginevyo,” alisema Sheikh Nasoro.

Sheikh Nasoro aliwata vijana kuwaheshimu wazazi wao wote wawili na ndipo wanapopata Baraka za Mwenyezi Mungu kupitia wazazi wao hao na kuwa wanaposhindwa kuwaheshimu wanapata chukizo la Mungu na mafanikio yao kufungwa.

Aidha, Sheikh Nasoro aliwataka viongozi kuwa wazalendo na kulitumikia Taifa kwa uaminifu huku wawa na hofu ya Mungu na kuhakikisha wananchi wanapata haki zao.

Akizungumzia kitabu kilichoandikwa na Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakar Zuberi Bin Ali kinachoitwa ni Nani wa Kulaumiwa kuhusu Mmomonyoko wa maadili alisema wanaopaswa kulaumiwa ni viongozi wa dini na waumini wao na akasema kila mmoja wao anapaswa kuwa balozi katika kusimamia maadili katika jamii jambo litakaloondoa vitendo vya ushoga, ulawiti na mambo mengine yote ambayo ni chukizo kwa Mwenyezi Mungu.

Imamu wa msikiti huo, Said Chepe akizungumza.
Swala ikiendelea
Waumini wakiwa kwenye swala hiyo.
Swala ikiendelea,

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad