VIONGOZI WA SKAUTI TAIFA WAKUTANA NA MKURUGENZI MTENDAJI MANISPAA YA SINGIDA JESHI LUPEMBE - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Wednesday, 31 July 2024

VIONGOZI WA SKAUTI TAIFA WAKUTANA NA MKURUGENZI MTENDAJI MANISPAA YA SINGIDA JESHI LUPEMBE

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Singida, Jeshi Lupembe (wa pili kushoto) akiwa na viongozi waandamizi wa Chama cha Skauti Tanzania (TSA) waliomtembelea ofisini kwake Julai 31, 2024 wakiwa safari kwenda nchini Burundi.

...................................

Na Dotto Mwaibale, Singida

VIONGOZI Waandamizi wa Chama cha Skauti Tanzania (TSA) wakutana na Mkurugenzi Mtendaji wa Manspaa ya Singida wakiwa safarini kuelekea nchini Burundi.

Viongozi hao waandamizi ni Kamishna Mkuu Msaidizi Utawala Bora, Fredrick Nguma, Kamishna Mkuu Msaidizi, Maafa na Ubinadamu, Mwalimu Mary Anyitike na maafisa wengine ambao wameambatana nao katika safari hiyo.

Kamishna Mkuu Msaidizi, Maafa na Ubinadamu, Mwalimu Mary Anyitike akizungumza kuhusu safari hiyo alisema wanakwenda nchini Burundi kuiwakilisha nchi katika mkusanyiko mkubwa wa Skauti Afrika

(JAMBO REE)

“Nchi zote wanachama wa Skauti Afrika zitakutana na kufanya shughuli mbalimbali zikwemo za elimu na za Kiskauti na kuwa kusanyiko hilo litakuwa la siku 10 kuanzia Agosti 2, 2024  hadi Agosti 12, 2024 na kuwa kutoka Tanzania Skauti 30 watakwenda kuwawakilisha wenzao,” alisema Anyitike.

Anyitike alisema Skauti ni ndugu na popote pale wanapokutana wanakuwa wamoja kwa kila jambo kama alivyokuwa akifanya muasisi wa Skauti.

Kwa upande wake Kamishna Mkuu Msaidizi Utawala Bora, Fredrick Nguma alisema wamelazimika kumtembelea Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Singida, Jeshi Lupembe kwa kuwa naye ni Skauti Mwenzao hivyo lisingekuwa jambo la busara kupita Singida bila ya kumuona kamanda mwenza ambapo alitumia nafasi hiyo kumshukuru kwa mapokezi mazuri aliyowafanyia.

Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Jeshi Lupembe aliwashukuru viongozi hao waandamizi wa Skauti kwa kumtembelea ambapo walikumbushana mambo mengi yanayofaywa na Skauti na kueleza kuwa Manispaa ya Singida ina skauti ambao wanafanya vizuri na akawatakia safari njema na  ushiriki mzuri  katika kusanyiko hilo na kuwa watanzania wanategemea kupata mambo mazuri watakayopta kwenye kusanyiko hilo.

Viongozi hao wa Skauti na ujumbe wao wakimsikiliza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Singida( hayupo ) pichani wakati alipouwa akizungumza nao.
Maafisa wa Skauti kutoka Dar  es SalaamHamadi Mtaliya (kushoto) na Erickson Adams wakiwa katika katika mazungumzo na mkurugenzi huyo.
Skauti hao wakiondoka baada ya kufanya mazungumzo na mkurugenzi huyo.



 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad