.......................
Na Mwandishi wetu.
KAMISHNA Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Yusuph Mwenda amewataka
mawakala wa forodha nchini kufanya kazi kwa weledi, uadilifu na kujiepusha na
vitendo vya rushwa.
Mwenda amesema hayo, leo Julai Mosi, 2024 alipokutana na wanachama wa Chama
cha Mawakala wa Forodha (TAFFA) wakiongozwa na Rais wa Chama hicho, Edward Urio
kwa lengo la kusikiliza changamoto zao, kujadiliana namna ya kuzitatua na
kuboresha huduma za forodha ili kuhakisha wanalipa kodi stahiki na kwa hiyari.
Kikao hicho kimefanyikia katika ukumbi wa mikutano wa TPA, jijini Dar es
Salaam.
Aidha kamisha amewahakikishia wanachama hao kuwa ameyachukua maoni yao na
changamoto kwa yale yaliyokuwemo ndani ya uwezo wao watakwenda kuyafanyia kazi
na yale ya kisera watayapeleka sehemu husika.
Naye, Rais wa TAFFA, Edward Urio amesema kuwa ushirikiano wao na maofisa wa
idara ya forodha umeifanya idara hiyo kuvuka malengo walioyowekewa katika
ukusanyaji kodi kwa mwaka fedha 2023/2024.
"Mamlaka ya Mapato (TRA) kupitia idara ya forodha walivuka malengo ya
ukusanyaji wa kodi kutoka na ushirikiano mzuri wa kati ya maofisa wa TRA na
sisi mawakala wa forodha"
"Sisi mawakala wa forodha ni sehemu ya ushirikiano na TRA kwenye
kukusanya kodi kwa niaba ya serikali "
Amesema kuwa mawakala wa forodha wamefurahi kuona namna ambavyo Kamishna
Mkuu wa TRA alivyoona umuhimu wao kwa kukubali kukutana nao kwa ajili ya
kujadiliana namna ya kuongeza usanifu wa ukusanyaji kodi na kuboresha
ushirikiano .
"Tunamhakikishia Kamishna Mkuu kuwa malengo aliyopewa si yake pakee
yake tutashirikiana naye kuhakikisha yanatimia"














No comments:
Post a Comment