AFISA TARAFA SINGIDA AAGIZA KUSIMAMISHA UJENZI ENEO LINALODAIWA KUWA LA MSIKITI - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Saturday, 3 August 2024

AFISA TARAFA SINGIDA AAGIZA KUSIMAMISHA UJENZI ENEO LINALODAIWA KUWA LA MSIKITI

Sheikh wa Mkoa wa Singida, Issa Nasoro akizungumza na Waislamu wa Msikiti wa Munawara kuhusu mal za Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) zinavyo hujumiwa.

.................................

Na Dotto Mwaibale

AFISA Tarafa ya Mungumaji katika Manispaa ya Singida, Othman Mzee amepiga marufuku shughuli zote za ujenzi zinazofanyika katika eneo la Msikiti wa Masjid Munawara uliopo Kata ya Misuna zinazodaiwa kufanywa na watu wanaotajwa kuwa ni wavamizi.

Mzee alitoa agizo hilo alipofika kuzungumza na waumini wa dini ya kiislamu baaa ya swala ya Ijumaa iliyofanyika jana katika msikiti huo kufuatia mgogoro wa ardhi uliopo baadhi ya watu wanaodai kuwa eneo hilo ni lao.

" Ninatoa maagizo ya kusimamisha shughuli zote za ujenzi kwenye eneo hilo na mtu yeyote anayedai kuwa eneo hilo ni la kwake nawaomba kuanzia jumatatu wafik ofisi kwangu wawe na nyaraka zinazoonesha kuwa eneo hilo ni lake," alisema Mzee.

Sheikh wa Mkoa wa Singida, Issa Nasoro akizungumza wakati wa ibada ya swala ya Ijumaa aisema kumekuwe na changamoto ya mali za kislamuzilizopo chini ya Baraza Kla Kiislamu )BAKWAA) Mkoa wa Singida kuvamiwa na watu ambao hawana hofu ya Mungu.

Alisema  wnaovaovamia maeneo hayo ni waislamu wenyewe ambapo alieleza kuwa mali zote za waislamu zipo chini ya Baraza la Wadhamini na si vinginevyo

Sheikh wa Kata ya Misuna, Omari Is-Haka alisema kumekuwa na changamo kubwa ya watu kuvamia maeneo ya msikiti iliyopo chini ya BAKWATA jambo ambalo halikubaliki.

Alisema maeneo yote ambayo yanavamiwa ni mali halali ya BAKWATA na kuwa yana nyaraka na hatimiliki.

Omari Lissu ambaye anadai kuwa maeneo hayo yanayodaiwa kuwa ni ya BAKWATA ni ya kwao na yalikuwa yakimilikiwa na babu zake wanne ambao amewataja kwa jina moja moja akianza na Digina, Mumwi, Mgiha na  Lissu ambaye i babu aliyemzaa baba yake.

Alisema kama familia eneo ulipojengwa msikiti na madrasa walilitoa kwa waislamu kama walivyoomba na Sheikh wa Mkoa wa Singida wa wakati huo, Sheikh Mahame lakini kuna eneo la Nasari bado ni la lao na ndilo wanalogombania

Lisu alisema anavielelezo vyote kuhusu eneo hilo mpaka ramani ambayo ipo ofisi ya ardhi mkoa na kuwa atasimama kidete kuhakikisha haki yao inapatikana kwani kuna baadhi ya watu wanania hofu ya kutaka kuwapoka eneo hilo alililoachiwa mama yao mwenye miaka 87 na baba yao Mzee Issa Lissu ambaye kwa sasa ni marehemu.

Aidha Lissu alikana familia hiyo kupewa viwanja 12 vilivyotolewa na ofisi ya ardhi kama mbadala wa eneo hilo ambalo lilipimwa kwa ajili ya taasis ya dini.

Afisa Tarafa ya Mungumaji katika Manispaa ya Singida, Othman Mzee, akizungumza 
Sheikh wa Kata ya Misuna, Omari Is-Haka akizungumza.
Afisa Tarafa ya Mungumaji, Othman Mzee akizungum na familia ambazo zinadai maeneo hayo ni yao.
Muonekano wa moja ya nyumba inayodaiwa kujengwa kwenye eneo la msikiti huo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad