............................
Imeandaliwa na Dotto Mwaibale, (0754-362990)
Uzalendo ni hali ya
mtu kuipenda, kuithamini na kujitoa kwa ajili ya nchi yake na Mzalendo wa kweli
anaweka maslahi ya nchi mbele na yake binafsi yanakuwa nyuma.
Mzalendo ni mtu
yeyote mzawa wa nchi husika na mwenye kuipenda na kujitoa mhanga na saa
nyingine ikibidi kufa kwa ajili ya nchi yake.
Uzalendo unabeba dhana pana ikianzia asili,
utamaduni, lugha, siasa, historia na kuwa dhana kuu ya uzalendo ni utaifa.
Kuna baadhi ya watu
licha ya kuwa ni wazalendo ambao wapo tayari kupoteza maisha yao kwa ajili ya
kutetea nchi yao uzalendo wao umekwenda mbali zaidi kwa kujitoa kusaidia jamii bila ya kujali kipato
chao cha fedha walichonacho.
Hapa nchini tunao
viongozi wengi ambao ni wazalendo na waliokuwa wazalendo kama Hayati Baba wa
Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na wenzake wote waliombele za haki na wale ambao
bado wapo hai.
Leo napenda
kumuongelea David Mulokozi ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mati Super
Brands Ltd yenye makao makuu yake Babati
mkoani Manyara ambayo inazalisha na kusambaza vinywaji, pombe kali aina ya
Strong Dry Gin, Sed Pineapple Flavour Gin, Strong Coffee na Tanzanite Premium Vodka..
Mfanyabiashara huyu Bilionea ni mtu ambaye anajitoa kusaidia jamii na makundi mengine kutokana na uzalendo wake alionao na si vinginevyo kwani kuna baadhi ya watu wataweza kuibuka na kusema amekuwa akifanya hivyo kwa sababu ya utajiri wa fedha alionao.
Tumewaona
wafanyabiashara wengi aina ya Mulokozi ambao Mungu amewajaalia kuwa na fedha
lakini hawana uzalendo wowote kwa Taifa wala kusaidia jamii niseme tu kuwa
kutoa ni moyo wa kizalendo alionao mtu husika na wala sio utajiri.
David Mulokozi ni
Mfanyabiashara asiye na makuu ambaye anashirikiana na Serikali vizuri na
makundi mengine ya watu na katika kuunga mkono jitihada za Serikali chini ya
Rais Samia Suluhu Hassan kuhusu ajira kupitia kampuni yake hiyo ametoa ajira
zaidi ya 300.
Binafsi napenda
kusema kazi hii kubwa anayoifanya Mulokozi isibezwe bali aendelee kuungwa mkono
kwani katika maisha ya kila mtanzania mwenye ajira kwenye
familia yake hawapungui watu watano wanaomtegemea hivyo kupitia kampuni hiyo
kuna watu wengi ambao wananufaika nayo zaidi ya hao waliopo kwenye ajira.
Kutokana na
uzalendo huo mkubwa alionao Mulokozi kwa Taifa na jamii anatambulika na
Serikali kwa kulipa kodi stahiki na ndio maana wakati wote viongozi wa Serikali
na Chama Cha Mapinduzi wamekuwa wakiitembelea kampuni hiyo kuona uwekezaji
uliopo ambao una mchango mkubwa wa kuinua uchumi wa nchi na Mkoa wa Manyara kwa
ujumla.
Mulokozi kupitia
kampuni yake hiyo ya Mati Super Brands
Ltd amekuwa akijitoa kwa dhati ya moyo wake katika hali ya raha na shida
kusaidia jamii na makundi mengine hapa nieleze machache kati ya mengi ambayo
yamefanywa na kampuni hiyo chini ya Mkurugenzi huyo Bilionea Mulokozi.
Moja ya jambo kubwa lililowahi kufanywa na kampuni hiyo kupitia mkurugenzi huyo ni pale alipotoa msaada wa vyakula na vitakasa mikono kwa ajili ya kujikinga na virusi vya corona.
Vifaa vilivyo tolewa ni mchele, mafuta ya kula, sabuni na vitakasa mikono ambavyo vilotolewa kwenye vituo vya watoto yatima na wazee na vitakasa mikono kwa taasisi za serikali ambavyo vilipokelewa na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti.
Mbali ya kutoa msaada huo pia kuna misaada minginemingi amekuwa akiitoa kwa jamii na kwa makundi mengine ya watu wenye uhitaji.
Mkurugenzi Mulokozi ni mtu mwenye huruma na maono ya mbali kwenye shughuli zake, mbali ya kujitoa kwake huko pia amekuwa mpenzi wa michezo na burudani ambapo amekuwa akishiriki katika mabonaza mbalimbali kwa kuzingatia kuwa michezo ni afya.
Katika kupenda
michezo Mulokozi alizindua Tawi la mashabiki wa
timu ya Soka ya Fountain Gate FC Tawi la Babati mkoani humo likiwa na lengo la
kuhamasisha vijana kupenda michezo na kuiunga mkono timu hiyo iliyohamia Mjini
Babati katika Uwanja wa Tanzanite Kwaraa kutoka mkoani Mwanza.
Mulokozi alipongeza ubunifu wa vijana hao
wa kuanzisha tawi hilo ambapo aliahidi kupitia kampuni yake hiyo kuwasaidia.
Mulokozi katika tukio lingine la kuonesha
upendo ni lile alilolifanya la kutoa zawadi ya Bajaji mpya kwa
Dereva wa bajaji Abel Rajabu ambaye alibandika picha ya Bilionea huyo kwenye
bajaji yake baada ya kuvutiwa na kazi anazozifanya za kuwekeza kwenye viwanda
na kusaidia jamii inayomzunguka kutokana na faida anayoipata.
Kutokana na kufanya vizuri kampuni hiyo
imekuwa ikipongezwa na wadau ambao wamekuwa wakitambua mchango wake ambapo Taasisi ya Kijeshi ya Command and Staff college ilitoa tuzo kwa kampuni
hiyo kutokana mchango mkubwa ilioutoa kwa taasisi hiyo.
Taasisi hiyo
ilitunukiwa tuzo hiyo kutokana na mchango wake mkubwa ilioutoa wakati wa mafunzo ya maofisa
wa jeshi kutoka nchi mbalimbali waliyoyapata kwenye ziara maalumu ya kimafunzo
kupitia kampuni hiyo ya Mati Super Brands Ltd.
Akipokea tuzo hiyo
Mulokozi alisema imewapa heshima kubwa na nguvu ya kuendelea kufanya kazi kwa
bidii hasa zile zizazohusisha jamii.
Mafanikio hayo
makubwa yanayopatikana ndani ya kampuni
hiyo hayapatikani hivi hivi bali yanatokana na uongozi mzuri wa Bilionea
Mulokozi na timu yake ya watendaji kazi ambao wamekuwa wakiwezesha nyenzo
mbalimbali za kazi ikiwa ni pamoja na kupatiwa zawadi na motisha kwa
wafanyakazi bora.
Binafsi napenda
kukuambia Mulokozi kazi unayoifanya inaonekana na jamii nzima ya watanzania hivyo
endelea kuifanya kama unavyowiwa huku ukielewa kuwa hakuna kazi isiyo na
changamoto Mungu aendelee kukupa afya njema na uendelee kuwatumikia wana
Manyara na Taifa kwa ujumla tukijua kuwa wafanyakazi wote uliowapa ajira katika
kampuni yako wanatoka mikoa mbalimbali hapa nchini. Kazi Iendelee.
Mmoja wa Viongozi wa Taasisi ya Kijeshi ya Command and staff College alipokuwa akimkabidhi tuzo Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mati Super Brands LTD, David Mulokozi kutokana mchango mkubwa aliounyesha kwa taasisi hiyo.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Mati Super Brands
Limited, David Mulokozi akipokea Certificate of Recognition kutoka Jeshi la Police Tanzania
Mkoa wa Manyara. Kulia anayekabidhi cheti hicho ni aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti.
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mhe. Makongoro Nyerere (kulia) akipata maelezo kutoka kwa mkurugenzi wa kampuni hiyo, David Mulokozi wakati alipotembelea kiwanda hicho.
Viongozi mbalimbali wa Taasisi ya Kijeshi ya Command and Staff College wakiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Kampuni ya Mati Super Brands LTD baada ya taasisi hiyo kuitunuku tuzo ya heshima kampuni hiyo.














No comments:
Post a Comment