Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mbunge wa Mufindi
Kusini, David Kihenzile amepata nafasi ya kuzungumza na wanasoka katika kijiji
cha Ihowanza, Wilayani Mufindi akiwataka wasisahau kujiandikisha kwenye daftari
la makazi.
Kihenzile amekuwa na ziara ya kata kwa kata
katika Jimbo lake akihamasisha wananchi kujiandikisha.
Akizungumza na wananchi wa Ihowanza, Kihenzile
amesema "Tunahitaji viongozi Bora
na wachapakazi kuanzia ngazi ya Vijiji, Vitongoji na Mitaa hivyo basi tunapaswa
kujiandikisha mapema kwenye daftari la mkaazi ili tuweze kupata nafasi hiyo ya
kushiriki katika uchaguzi wa Serikali za mitaa hapo Novemba 27," amesema.
Mbali na mambo mengine Kihenzile amempongeza
juhudi kubwa za kuibua vipaji kupitia mabonanza yenye ujumbe mahususi wenye
kuhamasisha uchaguzi wa Serikali za mitaa.
Aidha amewataka Wananchi hao kuendelea kumuombea
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassani pindi
anapotekeleza majukumu yake kwa maslahi mapana ya Wananchi wa Kata hiyo na
Jimbo kwa ujumla.
Hivi karibuni Kihenzile alifanya bonanza kubwa
katika bonde la Mgololo lililojumuisha Kata zote tatu ikiwemo Kiyowela, Idete
na Makungu na kugawa zawadi nono na vifaa mbali mbali vya michezo kwa washindi.
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mbunge wa Mufindi Kusini, David Kihenzile (katikati) akiwa na wanamichezo wa jimbo lake na wanannchi wakati wa uhamasishaji wa kujiandikisha kwa kutumia soka.
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mbunge wa Mufindi Kusini, David Kihenzile akizungumza na wananchi wa jimbo lake kupitia michezo wakati wa uhamasishaji huo.

No comments:
Post a Comment