Na Mwandishi Wetu
SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kupitia Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo imeingia makubaliano ya
kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika sekta ya
Michezo.
Makubaliano hayo yameingiwa Oktoba 19, 2024 Jijini Dar es Salaam kupitia
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro na Jamhuri ya
Kiislam ya Iran ikiwakilishwa na Mhe. Gholamreza Nouri Waziri wa Kilimo.
Nchi hizo zinatarajia kushirikiana katika Utalii wa michezo, kubadilishana
wataalamu pamoja na kupeana uzoefu katika miundombinu ya michezo.
Hafla hiyo imehudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki Mhe. Balozi Mahmood Thabit Kombo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni,
Sanaa na Michezo Bw. Gerson Msigwa pamoja na wataalam wengine kutoka wizara
hizo.









No comments:
Post a Comment