Msajili wa Hazina Bw. Nehemiah Mchechu (Kulia) akipata maelezo kutoka kwa
mwanafunzi wa Shahada ya Uzamivu (PhD) Henry Kahimba (Kushoto) alipotembelea
Maabara ya Taasisi hiyo.Na Mwandishi Wetu
Msajili wa Hazina Bw. Nehemiah Mchechu aipongezi Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela kwa kufanya vizuri katika tafiti na bunifu mbalimbali zinazotatua changamoto za jamii na kuchangia katika uchumi wa viwanda.
Akizungumza na menejimenti ya taasisi hiyo katika ziara yake Oktoba 21, 2024 Tengeru jijini Arusha ambapo ameeleza kuwa Taasisi hiyo inapaswa kuangaliwa kwa jicho la umuhimu ili kuongeza uzalishaji wa bunifu mbalimbali kupitia tafiti zinazofanyika.
“Taasisi hii ni ya kipekee , ili maendeleo yaweze kupatikana lazima sayansi na Teknolojia ihusike" anasema Mchechu.
Anazidi kueleza kuwa, Ofisi ya Msajili wa Hazina inaangalia namna ya kuanzisha kitengo kitakachounganisha watafiti, uhamasishaji rasimali na ubiasharishaji ili kuwezesha tafiti zinazofanyika kuwafikia walengwa hivyo kukuza uchumi wa Taasisi na nchi.
Naye Makamu Mkuu wa Taasisi hiyo, Prof. Maulilio Kipanyula ameeleza kuwa, ziara ya Msajili wa Hazina ni muendelezo katika kuleta mageuzi ya kiutendaji katika taasisi za umma ikiwemo taasisi ya Nelson Mandela ambayo ni kiota cha sayansi , teknolojia na ubunifu katika kuleta mageuzi ya kiuchumi ndani na nje ya nchi kupitia bunifu zake.
Msajili wa Hazina Bw. Nehemiah Mchechu alipata wasaa wa kutembelea maeneo mbalimbali ya kimkakati ikiwemo Kituo cha Elimu Kuditali (C-CoDE) maktaba, Maabara, kituo cha tehama (HPC),kituo Atamizi (Incubation Centre), Kiwanda kidogo (DDI) pamoja na mradi wa ujenzi wa mabweni ya wanafunzi.
Msajili wa Hazina Bw. Nehemiah Mchechu (Kulia) akipata maelezo kutoka kwa
mwanafunzi wa Shahada ya Uzamivu (PhD) Henry Kahimba (Kushoto) alipotembelea
Maabara ya Taasisi hiyo.
Msajili ya Hazina Bw. Nehemiah Mchechu (aliyekaa) akipata maelezo kutoka
kwa Afisa Uhusiano Bw. Octavian Kanyengele ( kushoto) namna elimu kidigitali
inavyotolewa katika kituo cha elimu ya kidigitali ( C-CoDE) kilichopo katika
Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Oktoba 21, 2024
kulia ni Makamu Mkuu wa Taasisi Prof Maulilio Kipanyula.
Msajili wa Hazina Bw. Nehemiah Mchechu (katikati) akipata maelezo kuhusu
mashine ya kisasa ya kuchakata uchafu na kuzalisha mbolea na gesi asilia kutoka
kwa Mwanafunzi wa Shahada ya Uzamivu Petro Mwamlima (kulia) katika kituo cha
Atamizi Oktoba 21, 2024, Kushoto ni Makamu Mkuu wa Taasisi Prof. Maulilo
Kipanyula.
Msajili wa Hazina Bw. Nehemiah Mchechu (katikati) akipata maelezo kutoka
kwa Mtafiti Msaidizi wa Chakula na Lishe Kelvin Vulla (Kushoto) wakati
alipotembelea kiwanda kidogo cha DDI Oktoba 21, 2024 kulia ni Makamu Mkuu wa
Taasisi Prof. Maulilio Kipanyula.
Msajili wa Hazina Bw. Nehemiah Mchechu (wa pili kulia) akisisitiza jambo
alipotembelea mradi wa ujenzi wa mabweni ya wanafunzi katika Taasisi ya Afrika
ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Oktoba 21, 2024 , wa pili kushoto ni Makamu
Mkuu wa Taasisi Prof Maulilio Kipanyula, Meneja Milki Ing. Willyhardus Karumuna
( wa kwanza kushoto) .









No comments:
Post a Comment