Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Maryprisca Mahundi akishuhudia utiliaji saini makubaliano uliofanywa leo Oktoba 21, 2024 na Wizara hiyo na Kampuni ya uwekezaji wa Kampuni ya huduma za mawasiliano ya Kielekroniki ya China (CECIS). Makubaliano hayo yamesainiwa na Katibu Mkuu Wizara hiyo Bw. Mohammed Abdulla na Mwenyekiti wa Kampuni ya CECIS Bw. Guo Zhaoping ambapo kupitia makubaliano hayo makampuni zaidi ya 600 ya kutengeneza komputa na vifaa vyake yataweza kuwekeza nchini Tanzania.
.................................
Na Grace Semfuko, Maelezo.
Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, leo Oktoba 21, 2024,
imetiliana saini makubaliano ya uwekezaji na mafunzo na Kampuni ya Huduma za
Mawasiliano ya Kielekroniki ya China (CECIS LTD) ambapo kupitia makubaliano
hayo, zaidi ya makampuni 600 ya vifaa vya kompuya yataweza kuwekeza nchini.
Lengo la uwekezaji huo ni kuongeza ujuzi kwa vijana na kuifanya Tanzania
kuwa kitovu cha utengenezaji wa kompuya kimataifa.
Makubaliano hayo yamesainiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,
Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Bw. Mohammed Abdulla na Mwenyekiti wa
Kampuni ya Huduma za Mawasiliano ya Kielekroniki ya China CECIS Bw. Guo
Zhaoping na kushuhudiwa na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Maryprisca Mahundi
ambaye amesema Tanzania inakwenda kupiga hatua kubwa katika masuala ya uchumi
wa kidijitali.
"Makubaliano haya ni matokeo ya ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan
nchini China aliyoifanya hivi karibuni, Kampuni hii ni wabobezi wa masuala ya
usalama wa mitandao hivyo elimu waliyonayo itawawezesha vijana kujifunza kwani
tunahitaji wataalam wengi zaidi wa TEHAMA nchini" amesema Mhe. Mahundi.
Nae Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari
Bw. Mohammed Abdulla amesema uwekezaji huo utatoa fursa kwa watanzania
kujifunza na kupata ajira.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kampuni ya huduma za mawasiliano ya
kielekroniki ambaye pia ni Naibu Mkurugenzi wa Sayansi na Teknolojia wa Kamati
ya Kampuni hiyo Bw. Guo Zhaoping amesema uwekezaji huo umefuata misingi ya nchi
za Tanzania na China na kwamba unalenga kuchochea maendeleo ya uchumi wa
kidijitali.
"Kampuni yetu inafanya uwekezaji katika mambo makuu matano ikiwepo
sekta ya kompuya na usalama wa mitandao ambapo pamoja na kufanya shughuli za
kibiashara pia tunalenga kukuza uchumi wa kidijitali baina yetu na nchi
zingine, kwa hapa Tanzania tutafanya kazi kulingana na mahitaji" amesema
Bw. Zhaoping.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya TEHAMA Dkt. Nkundwe Moses Mwasaga amesema pamoja
na mambo mengine, pia wamekubaliana kuvutia makampuni mbalimbali ya
Kielekroniki kuwekeza nchini ambapo mwaka 2025 kutakuwa na maonesho makubwa ya
utengenezaji wa vifaa vya kompuya Afrika ambapo Wizara ya Habari, Mawasiliano
na Teknolojia ya Habari kupitia Tume yake watakuwa wenyeji wa maonesho hayo.
Makubaliano hayo yamesainiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,
Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Bw. Mohammed Abdulla na Mwenyekiti wa
Kampuni ya huduma za Mawasiliano ya Kielekroniki ya China (CECIS) Bw. Guo
Zhaoping.
Mikataba hiyo ikioneshwa baada ya kusainiwa.









No comments:
Post a Comment