DC MAPUNDA, MD SATURA MEZANI NA WAFANYABIASHARA TEMEKE - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Saturday, February 22, 2025

DC MAPUNDA, MD SATURA MEZANI NA WAFANYABIASHARA TEMEKE

Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe.Sixtus Mapunda akiambatana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke Ndg. Jomaary Satura leo Februari 22, 2025 wameketi pamoja na Wafanyabiashara wa Temeke ikiwemo Viongozi wao kwa ngazi ya Wilaya, Mkoa na Taifa lengo likiwa ni kusikiliza changamoto zao na kuzipatia utatuzi.

Mkutano huo uliobeba pia Agenda ya kukumbushana na kusisitizana umuhimu wa kulipa Kodi Stahiki kwa wakati ili kurahisisha jukumu la Serikali katika kuwaleta Wananchi Maendeleo umefanyika katika Viwanja vya CCM Temeke Mwisho ukihudhuriwa pia na wataalamu kutoka Manispaa ya Temeke.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad