VIONGOZI ITIGI WAKUTANA NA VIKUNDI VYA WANAWAKE KWA AJILI YA MAANDALIZI YA SIKU YAO - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Saturday, February 22, 2025

VIONGOZI ITIGI WAKUTANA NA VIKUNDI VYA WANAWAKE KWA AJILI YA MAANDALIZI YA SIKU YAO

Viongozi wa Kata ya Itigi Mjini, wakiwa katika picha ya pamoja na wanawake wajasiriamali wa kata baada ya kufanya kikao cha maandalizi ya maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani ambayo yatafanyika Machi 5, 2025

.................................................
 

Na Dotto Mwaibale, Singida

VIONGOZI mbalimbali wa Kata ya Itigi Mjini wamekutana na vikundi kadhaa vya wanawake wa kata hiyo  kwa ajili ya maandalizi ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yatakayo fanyika March 5, 2025 kwa ngazi ya Halmashauri.

Viongozi hao waliokutana na vikundi hivyo ni Diwani wa Kata ya Itigi Mjini Mhe.Ally Minja, Afisa Mtendaji wa kata hiyo,  Saimoni  Sirilo na Mbuva Mwenda (Cdo)

Diwani wa Kata hiyo Ally Minja akizungumza na waandishi wa habari alisema wameamua kukutana na kundi hilo kwa lengo la kujadili mambo kadhaa ikiwa ni maandalizi ya maadhimisho ya siku yao hiyo ambayo yatafanyika duniani kote.

“ Kama viongozi wa kata hii na umuhimu wa maadhimisho hayo licha ya kuwa sio siku yetu tumeona ni vizuri tukutane nao tuweze kupanga mambo kadhaa ikiwa ni maandalizi kuelekea maadhimisho hayo ambayo yataambata na shughuli mbalimbali za kundi hilo la wanawake ambapo pia kutakuwa na maonyesho ya bidhaa zao,” alisema Minja.

Mwezeshaji maarufu wa ujasiriamali kwa wanawake hao na makundi mengine katika wilaya hiyo na Mkoa wa Singida kwa ujumla, Saimoni Sirilo alisema dhamira yao ni kuendelea kuwajengea uwezo na kuwapa mafunzo ya utengenezaji wa bidhaa bora na nzuri ili waweze kuibuka washindi katika maonesho hayo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad