CHAWATA WAMPONGEZA RAIS SAMIA UBORESHAJI HUDUMA ZAO - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Monday, 24 March 2025

CHAWATA WAMPONGEZA RAIS SAMIA UBORESHAJI HUDUMA ZAO

Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu Mkoa wa Dar es Salaam, Charles Matemba, akizngumza katika mkutano na waandishi wa habari Machi 24, 2025 Makao Makuu ya Chama cha Walemavu Tanzania (CHAWATA) Buguruni Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Chawata, Wilaya ya Ubungo, Athumani Sembe.

....................................

Na Dotto Mwaibale, Dar es Salaam

CHAMA cha Walemavu Tanzania (CHAWATA) Mkoa wa Dar es Salaam kimempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha huduma za walemavu ikiwemo mkopo wanaokopeshwa kuanzia mtu mmoja.

Akizungumza na waandishi wa habari Machi 24, 2025, Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu Mkoa wa Dar es Salaam, Charles Matemba alisema Rais Samia amewaboreshea huduma ukiwemo ushirikishwaji katika masuala mbalimbali.

“ Katika kipindi hiki cha miaka minne ya uongozi wake walemavu tumekuwa tukipata fursa za kushiriki semina na kuhudhuria makongamo na hasa kushirikishwa kwenye mchakato mzima wa uchaguzi jambo ambalo ni kubwa na la heshima kwetu,” alisema Matemba.

Akielezea baadhi ya changamoto walizonazo ni kukosekana kwa vifaa saidizi kwa kundi hilo ambapo ameomba Serikali kulifanyia kazi jambo hilo na kuomba ushirikishwa zaidi katika masuala ya maamuzi.

Mwenyekiti wa Chawata, Wilaya ya Kinondoni , Subira Semsimbazi akizungumzia suala la mikopo ya asilimia nne kwa kundi lao aliishukuru Serikali kwa mikopo hiyo ambayo imekuwa ikiwasaidia kukuza mitaji yao ya biashara na akatoa ushauri kwa wanawake wenzao kuitumia vizuri.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chawata, Wilaya ya Ubungo, Athumani Sembe alisema changamoto kubwa waliyonayo hawana ofisi zaidi ya kuahidiwa tu na kuelezea kuwa wanawake wenye watoto wenye ulemavu wasaidiwe na Serikali.

Mwakilishi wa vijana wenye ulemavu, Furaha Khalid alisisitiza kutolewa kwa elimu ya fedha kwa vijana kabla ya kupatiwa mikopo na kuwa semina hizo zitolewe mara kwa mara na si  pale tu wanapokopeshwa.

Naye Katibu wa Chawata Wilaya ya Kinondoni, Said Machaku aliwaomba waliokopo mikopo hiyo waweze kuirudisha na akaomba utaratibu wa kukopesha bajaji moja watu watano kuwa hauna afya kwa wakopaji hivyo aliomba babaji moja ikopeshwe mtu mmoja ili mkopo huo uweze kuwa na tija kwa muhusika.

Katibu wa Chawata, Wilaya ya Ubungo, Athumani Lubandame alisema mkopo huo wa asilimia mbili wanapaswa wakopeshwaji wapatiwe semina na kusisitiza mkopo huo apewe mtu husika baada ya kufundishwa stadi za uzalishaji.

Mwenyekiti wa Chawata, Wilaya ya Kinondoni , Subira Semsimbazi, akizungumza kwenye mkutano huo na waandishi wa habari.
Katibu wa Chawata, Wilaya ya Ubungo, Athumani Lubandame, akichangia jambo kwenye mkutano huo. Kulia ni Mwenyekiti wa Chawata, Wilaya ya Ubungo, Athumani Sembe.

Mkutano huo ukiendelea. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Chawata, Wilaya ya Kinondoni , Subira Semsimbazi, Katibu wa chama hicho Kinondoni, Saidi Machaku na Mtunza Hazina wa chama hicho Mkoa wa Dar es Salaam, Furaha Khalidi
Mkutano ukiendelea.
Viongozi mbalimbali wa Chawata wakiwa kwenye mkutano huo.


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad