DEREVA ALIYESABABISHA KIFO CHA OCD CHICO, ATIWA MBARONI, POLISI DAR KUIMARISHA ULINZI SIKUKUU YA EID - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Sunday, 30 March 2025

DEREVA ALIYESABABISHA KIFO CHA OCD CHICO, ATIWA MBARONI, POLISI DAR KUIMARISHA ULINZI SIKUKUU YA EID


Wazazi, Walezi watakiwa kuwachunga watoto wao

 Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam ,SACP Muliro Jumanne Muliro akizungumza na Wanahabari Machi 29, 2025.

...............................................

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

JESHI la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam limetoa  wito kwa wazazi na walezi kutowaacha watoto kwenda katika kumbi na maeneo mbalimbali bila kuwa na uangalizi kwani kufanya hivyo kunaweza kupelekea watoto kupotea,kupata ajali au kufanyiwa  vitendo vinavyoweza kuhatarisha afya na maisha yao.

Hayo yamebainishwa Machi 30,2025,Jijini  Dar es Salaam na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam ,SACP Muliro Jumanne Muliro wakati akizungumza na wanahabari amesema kwa kushirikiana na wananchi na vyombo vingine vya dola linaendelea kuimarisha usalama na linapenda kuwafahamisha wakazi wa Dar es Salaam kuwa Jiji lipo shwari.

Aidha,amesema Polisi Dar es Salaam inatambua kuwa tarehe 31,Machi 2025 au Aprili 1,2025 kutakuwa na sikukuu ya Eld-el-fitri kutegemea kuandama kwa mwezi.Kutokana na umuhimu wa sikukuu hiyo ,suala la usalama limewekewa uzito mkubwa katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam zikiwemo,fukwe za bahari ili sikukuu hiyo isherehekewe kwa amani na utulivu.

Hata hivyo Jeshi la Polisi halitasita kuchukua hatua kali za kisheria kwa dalili za vitendo vyovyote vya kijinai au vile vya usalama barabarani kwa madereva wote wa vyombo vya moto wenye tabia ya kupuuza na kukiuka sheria na usalama barabarani.

Sambamba na hayo,Jeshi la Polisi limemkamata EliaAswile Mbugi (maarufu kama Dogobata) Mnyakyusa (25),mkazi za Segerea dereva aliyekuwa aliendesha gari namba T 580 EAE aina ya TATA ambaye alitoroka Machi 17,2025 mara baada ya kusababisha ajali iliyosababisha kifo cha SP Awadh Ramadhani Chico aliyekuwa Mkuu wa Polisi Wilaya ya kipolisi Chanika.

"Mtuhumiwa huyo alikamatwa na makachero wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam tarehe 27 ,Machi 2025 huko maeneo ya Mbalizi Mkoani Mbeya,atafikishwa mahakamani haraka iwezekenavyo", alisema SACP Muliro.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad