SWALA YA EID SINGIDA KUFANYIKA VIWANJA VYA BOMBADIA - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Sunday, 30 March 2025

SWALA YA EID SINGIDA KUFANYIKA VIWANJA VYA BOMBADIA

Sheikh wa Mkoa wa Singida, Issa Nasoro akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Machi 29, 2025 Sikuku ya Eid al-Fitr itakayofanyika kesho.

.......................................

Na Solomon  Philemon, Singida

WAISLAMU Singida kusherehekea Sikukuu ya Eid al-Fitr   viwanja vya Bombadia ambapo swala ya iddi itafanyika hapo pamoja na mambo mengine.

Hayo yamebainishwa na Sheikh wa Mkoa wa Singida, Issa Nasoro wakati akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari ofisini kwake Machi 29, 2025 mjini Singida.

“ Niwasihi Waislam wote wa Manispaa ya Singida mfike mapema kwenye viwanja hivyo kwa ajili ya swala ya iddi ambayo itafanyika saa tatu kamili na baada ya hapo watu watatawanyika kwenda kusherehekea sikukuu hiyo majumbani mwao,” alisema Sheikh Nasoro.

Sheikh Nasoro aliwataka Waislam mkoani hapa kusherehekea sikukuu hiyo kwa salama na Amani huku akihimiza kuwalinda watoto na kuacha usalama kwenye nyumba zao watakapo kuwa sehemu tofauti tofauti kusherehekea sikukuu hiyo kwani wezi nao wanatumia nafasi hiyo kwenda kuiba.

Aidha, Sheikh Nasoro aliwaomba wafanyabiashara kushusha bei ya vyakula na nguo wakati huu wa sikukuu ili watu wasio na uwezo waweze kununua na kuwavika watoto hao jambo ambalo litawafanya kupata fadhira ya Mwenyezi Mungu.

Sheikh Nasoro aliwataka Waislam mkoani hapa kutosherehekea sikukuu hiyo kwa kunywa pombe, kufanya ufusika na matendo mengine yasiyo mpendeza Mwenyezi Mungu bali wayaishi matendo yote mema waliyoyafanya wakati wa kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad