......................................
Na Mwandishi Wetu, Njombe
Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Anthony Mtaka, amewataka watumishi wa umma kuwaheshimu wafanyabiashara na wadau wa sekta binafsi, akisisitiza kuwa mchango wao ni muhimu katika maendeleo ya mkoa na taifa kwa ujumla.
Mhe. Mtaka alitoa wito huo tarehe 24 Machi 2025, wakati wa uzinduzi wa Ofisi ya Kanda ya Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) mkoani Njombe, tukio ambalo lilihudhuriwa pia na Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo.
"Watumishi wa umma lazima tutambue kuwa sekta binafsi ni injini ya uchumi. Tuwaheshimu wafanyabiashara, tushirikiane nao, na kuhakikisha mazingira ya uwekezaji yanakuwa rafiki kwa maendeleo ya Njombe," alisema Mhe. Mtaka.









No comments:
Post a Comment