Mwakilishi wa Mtendaji Mkuu wa TARURA, Mhandisi Ismail Mafita akifungua semina hiyo Machi 28, 2025. jJijini Dar es Salaam.
.........................................
Dotto Mwaibale na Angelina Mganga, Dar es Salaam
WAKALA wa Barabara Vijijini na Mijini Tanzania (TARURA) imeandaa semina maalumu
kwa ajili ya kuwajengea uwezo Jumuiya ya wanahabari mitandao ya kijamii Tanzania (JUMIKITA) ili waweze kujua
shughuli mbalimbali zinazofanywa na Tarura na kuziandika kwa
ufasaha kwa manufaa ya wananchi na Taifa kwa ujumla.
Moja ya mada kubwa ambayo itatolewa katika semina hiyo ni
ujenzi wa madaraja kwa kutumia teknolojia ya mawe ambayo ni nzuri na inatunza
mazingira mada ambayo itatolewa na Mratibu Ujenzi wa madaraja na barabara za
mawe Mhandisi Pharles Ngeleja.
Mada ya pili katika semina hiyo itahusu Uhifadhi wa barabara na mitaro sio jalala ambayo iliwezeshwa na Dkt. Makene Madoshi.
Dkt. Makene Madoshi akitoa mada kwenye semina hiyo
Mratibu Ujenzi wa madaraja na barabara za mawe Mhandisi Pharles Ngeleja. akitoa mada kwenye semina hiyo.Kaimu Meneja Mahusiano na Mawasiliano TARURA, Catherene Sungura akizungumza kwenye semina hiyo.
Wanahabari wakiwa kwenye semina hiyo.








No comments:
Post a Comment