JAMII BORA SERVICE NETWORK YAANDAA KONGAMANO LA SAYANSI JUU YA MAGONJWA YA MFUMO WA CHAKULA. - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Tuesday, April 15, 2025

JAMII BORA SERVICE NETWORK YAANDAA KONGAMANO LA SAYANSI JUU YA MAGONJWA YA MFUMO WA CHAKULA.

Mratibu wa Kongamano la Kisayansi juu ya Magojwa ya mfumo wa chakula " (GAESTROENTEROLOJIA ),  Muhidin Mahende (katikati), akizungumza kuhusu kongamano hilo.

...........................................

By Christopher Siwingwa 

Taasisi ya Jamii Bora Service Network, imeandaa kongamano la kisayansi juu ya Magojwa ya mfumo wa chakula " GAESTROENTEROLOJIA litakalofanyika jijini Dar es salaam tarehe 25 mei katika hospital ya Muhimbili.

Mratibu wa kongamano hilo, Muhidin Mahende, amesema kongamano hilo linatarajia kuwaweka wataalam mbali mbali wa afya wenye hamasa ya kujifunza na kujadili maendeleo ya hivi karibuni pamoja na muelekeo wa matibabu kwa wagonjwa wenye matatizo ya mfumo wa chakula.

Bwana Mahende amesema kongamano hilo linatarajia kuwa na mada zitakazo wasilishwa moja kwa moja na majopo ya mjadala ya kina zinazo husu masuala ya mfumo wa chakula na tiba zake.

Pia amewataka watanzania na wataalam wengine wa tiba ya afya shirikishi, wanafunzi wa kozi mbali mbali za afya, wafanyakazi wa hospital, wamililki wa hospital na wasambazaji wa madawa kuhudhuria kongamano hilo.

Pia kongamano hilo litafanyika katika mfumo wa aina mbili , ana kwa ana na mtandaoni, ili kuruhusi ushiriki wa watu walioko nje ya Dar es salaam na kutoka sehemu mbali mbali duniani.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad