GAVANA BWANKU AONGOZA KIKAO MAALUMU CHA UTENDAJI KAZI - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Tuesday, 22 April 2025

GAVANA BWANKU AONGOZA KIKAO MAALUMU CHA UTENDAJI KAZI

Wajadili ajenda za ulinzi na usalama, utatuzi wa kero za wananchi, ulinzi ardhi za vijiji n.k 

 Afisa Tarafa wa Tarafa ya Katerero iliyopo Bukoba mkoani Kagera Ndugu Bwanku M Bwanku alifanya Kikao kazi cha pamoja na watumishi ndani ya Tarafa kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali ya maendeleo ndani ya Tarafa kikijumuisha Watendaji wa Kata zote 11 zinazounda Tarafa ya Katerero, Watendaji wa Vijiji vyote 37, Polisi Kata na Maafisa Mifugo.

Kikao hicho kimefanyika kwenye Shule ya Msingi Lyamahoro A Kata ya Nyakibimbili na kwa pamoja kuweka mikakati madhubuti ya ulinzi na usalama ndani ya Tarafa, utatuzi wa migogoro ya wananchi kwa wakati, ulinzi wa ardhi za vijiji baada ya kuwepo kwa wimbi kubwa la uvamizi wa ardhi za vijiji na mengine mengi. 

Tarafa ya Katerero ina jumla ya kata 11, vijiji 37 na vitongoji 157. Kwenye kikao hicho mkakati uliwekwa kuhakikisha hali ya usalama inaendelea kuwa shwari hasa nyakati hizi Taifa likielekea kwenye Uchaguzi Mkuu baadae mwaka huu 2025.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad