Mkazi wa Kijiji cha Mkulu Wilaya ya Singida, Juma Mohamed Swalehe aliyechuchumaa, akiwa na katika picha ya pamoja na wenzake.
...............................................
Na Dotto Mwaibale, Dar es Salaam
MKAZI wa Kijiji cha Mkulu
Wilaya ya Singida, Juma Mohamed Swalehe ambaye amelazwa Taasisi ya Mifupa Muhimbili
(MOI) jijini Dar es Salaam kwa matibabu
baada ya kuanguka kwenye mti alipokwa
akilina asali Machi 27, 2025 anaomba msaada wa fedha za matibabu.
Hali ya mgonjwa huyo mwenye namba ya kupokelewa hospitalini hapo 4474017 na mwenye faili la matibabu namba 491432 imeelezwa bado siyo nzuri na bado anaendelea na matibabu kufuati uti wake wa mgongo kupata madhara.
Akizungumzia tukio hilo Sheikh Abtway Said Kumala ambaye pia
ni Mratibu Mkuu wa Msikiti wa Ibn Abass uliopo Kijiji cha Nduamghanga Mkulu Tarafa ya
Mgori Kata ya Mghunga Wilaya ya Singida alisema baada ya kuanguka na kuwa
katika hali mbaya alipelekwa Hospitali ya Makiungu iliyopo Wilaya ya Ikungi lakini
kutokana na hali yake kuwa mbaya alipewa rufaa kwenda Hospitali ya Taifa ya Muhimbili
(MNH) ambako anaendelea na matibabu.
“Tumeambiwa kuwa hali yake imekuwa ikibadilika na kupelekwa
mara kadhaa chumba cha wagonjwa mahututi lakini tunamshukuru Mwenyezi Mungu
madaktari wanampambania,” alisema Sheikh Kumala.
Alisema changamoto kubwa iliyopo ni fedha za matibabu
anazodaiwa ambapo awali alitakiwa kulipa Shilingi 900,000 ambazo walifanikiwa
kuzitoa baada ya ndugu na jamaa kuchangishana lakini sasa imetoka bili mpya
ambapo zinahitajika Sh.Milioni 2,314,780.00.
Amesema kutokana na bili hiyo na familia kutokuwa na uwezo
wa kuilipa wanawaomba wananchi na na wadau mbalimbali kusaidia kupatikana kiasi hicho cha
fedha kwa ajili ya mpendwa wao huyo aliyopo hospitalini ili aendelee kupatiwa
matibabu kwani hawezi kusimama zaidi ya kulala wakati wote.
Kumala amesema kwa mtu yeyote atakaye kuwa tayari kumsaidia
kada huyo wa CCM ambaye anaendelea kupata matibabu anaweza kuwasiliana naye kwa
namba 0762606042 au namba 0782011608 ili kujua namna ya kupokea msaada huo.
Ndugu zangu watanzania shimeshime tujitokeze kumsaidia
mwenzetu huyu kwa kutoa chochote tutakacho jaaliwa na Mwenyezi Mungu na
tutabarikiwa kwa utoaji wetu.










No comments:
Post a Comment