Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila wakati wa mfumo wa uvuvi wa kisasa utakaohusisha njia za kidigitali zitakazosaidia wavuvi kujua maeneo sahihi ya upatikanaji wa samaki.
...........................................
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.
SERIKALI kwa kushirikiana na Taasisi ya Sapphire wamezindua mfumo wa uvuvi wa kisasa utakaohusisha njia za kidigitali zitakazosaidia wavuvi kujua maeneo sahihi ya upatikanaji wa samaki pamoja na kutambua na kujua hali ya hewa kwa siku husika.
Akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa mfumo huo katika soko la samaki Feri Jijini Dar es Salaam, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Edwin Mhede amewataka wavuvi kujiunga katika mfumo huo utakaowawezesha kujiinua kiuchumi kupitia uvuvi wa kisasa.
Aidha ,amesema mfumo huo wa uvuvi wa kidigitali unaojulikana kama Vua na Uza Kidigitali ni njia bora italayomwezesha mvuvi kuvua kisasa na mfumo huo umeunganishwa na Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA), ili mvuvi aweze kujua hali ya hewa atakavyokuwa majini kabla ya kwenda kuvua.
Amesema wavuvi wamepata uhakika wa kuvua kutambua na kujua hali ya hewa na mahali samaki wanapopatikana kwa wingi.
Hata hivyo, ametoa maagizo kwa Mkurugenzi wa Jiji la Dar es, Elihuruma Mabelya kuhusu kuwatengenezea mazingira rafiki ya kupata mikopo.
"Tengenezeni mazingira rafiki ya kuwapatia mikopo hawa wavuvi kwa kuwa tayari wapo kwenye mifumo rasmi," amesema Dkt.Mhede.
Pia ametoa wito kwa wavuvi kujisajili kwa wingi kwani mfumo huo ni bure ili kuongeza ukubwa wa soko.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesema sekta ya uvuvi imeendelea kuchangia ukuaji wa mapato katika jiji la ilala hivyo uzinduzi wa mfumo huo utaongeza ufanisi katika sekta ya uvuvi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa soko la uvuvi la samaki feri Nassoro Mbaga amesema wanaishukuru serikali kwa kuja na mfumo huu wa Vua Uza na Nunua Samaki Kigiditali watatumia vyema mfumo huo ili kujiinua kiuchumi na kujiongezea kipato.
Shabani Ramadhani mvuvi wa soko la feria ameishukuru Serikali kwani mfumo huo utawasaidia wavuvi kuwa na uhakika wa kupata samaki bila kubahatisha
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Edwin Mhede (katikati) akielekeza jambo wakati wa zindzi huo.Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Edwin Mhede, mfmo huo.
Viongozi mbalimbali wakionesha samaki wakati za uzinduzi huo.











No comments:
Post a Comment