............................................
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MWENYEKITI Taifa wa Chama Cha Tanzania Labour Party (TLP) Richard Lyimo ametangaza kutia nia ya kuwania nafasi ya Ubunge katika Jimbo la Bunju .
Kauli hiyo ameitoa Aprili 3,2025 Jijini Dar es Salaam kwa mahojiano maalum na mwandishi wa Dmnews yaliyofanyika katika Ofisi za Chama hicho.
Mwenyekiti Lyimo amesema nimeamua kutia nia kugombea nafasi ya Ubunge kupitia Chama changu ili niweze kuwatumikia wakazi wa Bunju kwani ninalijua vizuri Jimbo hilo maana mimi ni mzaliwa wa maeneo hayo.
Aidha ,amesema maamuzi hayo yanataka kuleta mapinduzi ya maendeleo kwa wakazi wa Bunju ambayo hayajatekelezwa kwa miaka mingi na mbunge wa Jimbo hilo.
"Ninataka nifanye yale mambo yaliyoshindikana ambayo hayajafanywa siku nyingi na mbunge wa Jimbo hilo ili wananchi wajue vizuri wajibu na kazi anazozifanya mbunge",alisema Lyimo.
Ameeleza kuwa ahadi hizo ni kutengeneza Barabara za vumbi ili ziwekwe lami pia kutafuta zao la biashara ambalo litawasaidia wananchi kujipatia kipato na kujivunia.
Pia amesema kazi za mbunge ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma muhimu za kijamii katika maeneo husika pia kuhakikisha wananchi wanapata pembejeo za kilimo kwa muda uliopangwa.
Hata hivyo alisema kwamba shule nyingi hazina madawati yakutosha pamoja na madarasa hivyo nitahakikisha yanakuwepo madawati yatakayotosheleza kwa wanafunzi ili wasikae chini lakini pia kuwa na vituo vya afya vya kutosha ambavyo vyakutosha vitakavyo wahudumia wazee kwa kuwatibu bila malipo yoyote.
Sambamba na hayo Mwenyekiti Lyimo alisema TLP kina wagombea watatu wanaotarajia kuwania nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,hivyo Chama kinatarajia kufanya mkutano mkuu mwezi Mei kwa ajili ya kupitisha mgombea atakayesimamishwa na Chama hicho , mchakato ndani ya chama bado haujafanyika kumpitisha mgombea wa nafasi ya urais.
Sanjari na hayo Mwenyekiti Lyimo ameelezea hali ya suala la utekaji nchini kwamba ni suala la aibu sana kwa nchi yetu kwani inaweza kuleta uvunjifu wa amani wakati nchi yetu ni kisiwa Cha amani.
"Vyama vya upinzani,Chama tawala pamoja na Jeshi la Polisi ,tukio lolote linalofanyika Polisi wao wanafanya uchunguzi,upelelezi kubaini nini kimetokea na sababu gani na kuhabarisha umma hasa masuala ya utekaji ili umma ujue hasa utekaji, masuala haya siyo tu yanachafua Chama tawala kwa kuwa ndicho kinabeba Polisi,ila Polisi wanalaumiwa kuliko hiyo CCM yenyewe kwani wapo ndani ya Chama tawala",alisema Lyimo.
Aliendelea kwa kueleza kwamba katika mazingira ya kwanza ya elimu ya political sayansi yanaweza yakafanywa na serikali ya chama kwa maana yakumfanya mpinzani aogope kushiriki upinzani lakini pia yawezwa kufanywa na Chama Cha upinzani kwa kuwa kinataka blessing ya nchi na nje,kwa hiyo yanataka mataifa ya nje yaone kama wanaonewa wanauawa ili waongezewe nguvu yakupambana na mauji,asilimia 90 mpinzani ni kuhakikisha anatafuta mapungufu ya chama tawala ili zikubebe wewe uendelee kuwa katika sifa.
"Haya mambo ya upinzani kama yanafanyika kisiasa,kibiashara pengine hata wafanyabiashara wanaweza kufanya hayo mambo pia wanaweza wasiwe CCM wala Chama Cha upinzani lakini ikawa hata majambazi ama watu wenye nia ovu au nia mbaya na serikali hivyo wananchi tuepuke kueleza moja kwa moja tuhuma katika maeneo ambayo haujafanyika upelelezi ukagundua kama ndivyo ilivyo.
"Yoyote ambaye anahusika na masuala hayo tunaomba atafute njia nyingine yakufanya ili kufanikisha adhima yake aliyokuwa anaifikiria kuwa itamsaidia kwani watakao umia ni watanzania,wapiga kura kwani hii itatuweka mahali ambapo si salama kisiasa wala kiamani na kiulinzi katika nchi.








No comments:
Post a Comment