WAMILIKI WA BUCHA ZA NYAMA YA NGURUWE WATAKIWA KUZINGATIA USAFI - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Wednesday, 2 April 2025

WAMILIKI WA BUCHA ZA NYAMA YA NGURUWE WATAKIWA KUZINGATIA USAFI

Muonekano wa nyama ya nguruwe ikiwa katika bucha.

................................................

Na Mwandishi Wetu, Mbeya 

Bodi ya Nyama Tanzania imewataka wamiliki wa bucha za nyama ya nguruwe (kitimoto) jijini Mbeya kuhakikisha wanazingatia matumizi ya vifaa stahiki katika usafirishaji, uhifadhi, na ukataji wa nyama hiyo.

Aidha, bodi hiyo imewasisitiza wamiliki wa bucha kudumisha usafi wa mazingira na vifaa wanavyotumia ili kulinda afya za walaji na kuhakikisha nyama inasalia katika hali bora kwa matumizi ya binadamu. 

Wito huu unalenga kuboresha viwango vya usafi katika biashara ya nyama jijini Mbeya, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuhakikisha usalama wa chakula na afya kwa wananchi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad