Mwenyekiti wa Chama Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiongoza moja ya mkutano mkuu wa chama hicho Jijini Dodoma.
.................................................
Na Dotto Mwaibale, Dar es Salaam
JIJI la Dodoma linatarajiwa kung’arishwa na rangi ya kijani katika mkutano
mkuu maalumu wa wa siku mbili wa Chama Cha Mapinzuzi (CCM) ambao unatarajiwa
kufanyika kuanzia Mei 29, 2025 hadi Mei 30, 2025 katika ukumbi wa Kisasa wa Mikutano
wa Jakaya Kikwete Convetion Center uliopo Jijini humo.
Mkutano huo utahudhuriwa na wajumbe kutoka mikoa yote ya
Tanzania Bara na Visiwani pamoja na wananchi wakiwepo viongozi na wadau mbalimbali
watakao kuwa wamealikwa na chama hicho kikubwa cha siasa hapa nchini.
Ajenda kubwa ya mkutano huo ni kupokea taarifa ya
utekelezaji wa Ilani ya chama hicho ya mwaka 2020/ 2025 ambayo imefanya vizuri
kwa utekelezaji wa miradi mbalimbali na maeneo mengine ya maendeleo na kuzindua
Ilani ya chama hicho ya mwaka 2025/ 2030.
Mkutano huo utaongozwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa Dkt. Samia
Suluhu Hassan ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya
Katibu Mkuu Taifa wa chama hicho Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi na kuhudhuriwa na
viongozi mbalimbali wa chama hicho.
Jiji hilo litang’alishwa na vazi maalumu la chama hicho
ambalo ni la kijani na njano sambamba na bendera za rangi hiyo zitazokuwa
zikipepea kila kona ya jiji hilo kubwa lililopo katikakati ya nchi yetu Dodoma.
Kazi na Utu Tunasonga mbele.
Katibu Mkuu Taifa wa chama hicho Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi
Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi na Katibu Mkuu wa CCM Taifa wakionesha mshikamano baada ya kuteuliwa kuwa wagombea nafasi ya urais kupitia CCM huku Dkt. Nchimbi kuwa mgombea mwenza kwa nafasi ya makamu wa Rais wa Dkt. Samia.
Wajumbe wakishiriki moja ya mkutano mkuu Jijini Dodoma








No comments:
Post a Comment