Viongozi wa TK Movement wa Mikoa na Wilaya wakishiriki Semina ya siku mbili ya Kitaifa jijini Dodoma.
Semina hiyo mahsusi kuelekea uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu iliyoanza jana Mei 3, 2025 na kufikia tamati Mei 4, 2025 ilifunguliwa na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Taifa, Mhe. Ali Hapi ambaye alihimiza vijana kuendelea kujenga mshikamano na kuhakikisha chama hicho kinapata ushindi mnono.
Baadhi ya viongozi waliohudhuria semina hiyo kutoka mikoani na wilayani ni Mratibu wa TK Movement kutoka Wilaya ya Newala, Khalfan Mtuhi, Mratibu wa TK Movement wa Wilaya ya Itigi, Musa Marando, Mratibu wa TK Movement wa Wilaya ya Manyoni, Nimwindael Sima, Mratibu Msaidizi wa TK Movement Wilaya ya Ikungi, Ibrahimu Dude na Mratibu wa TK Movement wa Wilaya ya Ikungi Mkoa wa Singida, Hussein Mseule.
Aidha, semina hiyo iliambatana na uzinduzi wa Samia Soldier.
Wenye lengo la kuwashirikisha vijana mchakato wa uchaguzi pamoja na kugombea nafasi za uongozi.








No comments:
Post a Comment