.Yawaasa
watanzania kuchangamkia fursa migodini
Na Mwandishi
Wetu, Mwanza
Kampuni ya
Barrick Twiga imethibitisha kwa vitendo utekelezaji wa ushirikishwaji wa
watanzania katika sekta ya madini kwa kufanya manunuzi Tsh 1.5 trillioni ambapo
Tsh 1.2 trilioni 75% ilikwenda kwa makampuni ya watanzania wazawa kupitia
kanuni ya maudhui ya ndani (Local Content)
Akitoa
salamu kwa niaba ya wadhamini wa Jukwaa la nne la utekelezaji wa ushirikishwaji
wa watanzania katika sekta ya madini nchini unaofanyika jijini Mwanza, Mkuu wa
Kitengo cha Ugavi wa Barick North Mara, Enock Otieno alisema kwamba kwa
ushirikiano wa Wizara ya Madini, Tume ya Madini na wadau wengine wamefanikiwa
kutekeleza kwa vitendo kanuni ya maudhui ya ndani (Local Content)
“Kwa
kushirikiana na Wizara, Tume na wadau wengine tumefanya mikutano, warsha na
makongamano kadhaa ili kuhamasisha na kukuza uelewa wa watanzania katika
kushiriki kwenye shughuli za uchumi katika sekta ya madini ili kuchochea
mabadiliko Chanya ndani ya nchini,” alisema Otieno
Aliongeza
kwamba kampuni ya Barrick Twiga kwa kutambua madini ni maisha na utajiri
wanatekeleza mradi wa barabara kutoka Kahama hadi kakola kilomita 73 kwa kutoa
Tsh 83.36 billioni kwa minajili ya kuboresha miundombinu.
Mgodi wa
Barrick North Mara umesisitiza kwamba ipo tayari kupokea na kutumia bidhaa
zinazozalishwa hapa nchini lakini muhimu ziwe na viwango vinavyohitajika,
Otieno
alisema kwamba mgodi wa Barrick North Mara una fursa nyingi kwa ajili ya
watanzania wazawa ili waweze kushiriki kwenye sekta ya madini.
“tupo tayari
kupokea bidhaa zinazotokana na viwanda vya ndani ili umuhimu watanzania wajue
mahitaji na ubora wa bidhaa kwa sababu usalama na afya za wafanyakazi ndani
migodi ni kipaumbele cha kampuni ya Barrick katika migodi yake hapa nchini,”
aliongeza
Otieno
alisema kwamba tuna fursa nyingine ni uhitaji wa chuma kwenye mgodi wa Barrick
North Mara na hii ni fursa kwa watanzania kuchangamkia kwa sababu pia kuna
upatikanaji wa malighafi ya chuma kutoka Liganga.
Alifafanua
kwamba ni muhimu watanzania kuzingatia weledi na kuunganisha nguvu zao ili
kuweza kuanzisha viwanda vya chuma kwa sababu mahitaji ya malighafi hiyo
migodini ni kubwa mno na fursa ya kipekee kwa watanzania wazawa kuanza kukua
katika ukandarasi na huduma za migodini hapa nchini.
“Hii ni
fursa ya kipekee kwa watanzania wazawa kuanza kuingia kwenye sekta ya madini
kwa sababu fursa zinapatikana mpaka kwenye ya uchongaji miamba kwenye mashimo
ya chini bado kuna hitajika bidhaa na mitambo kwa ajili ya shughuli za
uchimbaji na cementi ,” alifafanua Otieno
Alisema
kwamba umuhimu kwa watanzania wazawa kuzingatia ubora wa bidhaa na uendelevu wa
usambazaji wa huduma husika ili kuweza kujenga uaminifu na uwezo kwa
wakandarasi wa ndani kwenye sekta ya madini hapa nchini.
Naye ,
Meneja Mahusiano ya Jamii,wa Barrick North Mara, Franscis Uhadi kupitia alisema
kwamba kampuni hiyo ya Barrick ambayo inamiliki migodi ya North Mara,
Bulyanhulu na Buzwagi ambao huo katika hatua za mwisho za ufugaji inaendelea
kutekeleza kanuni zote za Maudhui ya Ndani (Local Content) na Uwajibikaji kwa
Jamii (CSR).
“Kampuni ya
Barrick inatekeleza kwa vitendo ushirikishwaji wa watanzania kwenye sekta ya
madini kwa kufanya kazi na makampuni ya wazawa na kuendelea kuwajengea,”
“Jumla ya
makampuni ya ndani 706 imefanya kazi na migodi ya barrick na kuna makampuni 603
ni kampuni za wazawa na bado tutaendelea kufanya kazi na makampuni ya
kitanzania kama sehemu ya kuwajengea uwezo,” aliongeza
Kwa upande
wake, Mgeni rasmi wa Jukwaa hilo la nne la ushirikishwaji wa watanzania kwenye
sekta ya madini, Waziri wa Madini, ,
Anthony Mavunde alisema kwamba
sekta ya madini imeweza kuchangia 9.0 % ya pato la taifa mwaka jana.
“mafanikio
katika sekta ya madini ni makubwa na mpaka sasa ninavyozungumza sekta hii ya madini
imechangia Tsh 985 billioni kwenye mfuko mkuu wa serikali haya ni mafanikio
makubwa sana kwenye sekta ya madini,” alisema Mavunde.
Aliongeza
kwamba serikali ya awamu ya sita chini Dkt Samia Suluhu Hassan ilitoa maelekezo
ya kuweka akiba ya dhahabu na ndani ya miezi nane Benki kuu ya Taifa (BOT) ina
akiba ya dhahabu ya Tani 5.2.
“Sekta hii
ya madini inakua kwa kasi kubwa pamoja na mambo mengine kuna viwanda tisa
vinajengwa vya kuchakata na kusafisha dhahabu ili kukuza mnyororo wa dhamani,”
aliongeza Waziri Mavunde.
Waziri
Mavunde alisema kwamba katika utekelezaji wa ushirikishwaji wa watanzania
kwenye sekta ya madini kupitia kanuni ya maudhui ya ndani (Local content)
ambapo kuna watanzania 16,874 ambao wameajiriwa kwenye sekta ya madini hapa
nchini.
Alifafanua
zaidi kwamba ni muhimu watanzania ambao ni watoa huduma wazingatie weledi
kwenye kazi ya utaoji huduma migodini (compliance) na kujenga utamaduni wa
kushirikiana kwa kushikana mikono ili wafanye kazi kwa ufanisi zaidi.
“ndugu zangu
watanzania changamkieni hizi fursa kwenye sekta ya madini kwa kushirikiana na
serikali itaendelea kutengeneza mazingira mazuri kwa wazawa kuweza kufanya kazi
kwenye migodi na kuwajengewa uwezo pamoja na kuhakikisha kwamba taasisi za
fedha zinawakopesha,” alisisitiza
Naibu Katibu
Mkuu Wizara ya Madini, Msafiri Mbibo alisema kwamba sekta ya madini imeendelea
kuchangia mapato ya serikali, kutoa fursa za ajira kwa watanzania kupitia
maudhui ya ndani (Local content), kukuza ujuzi kwa wazawa na kuvutia uwekezaji
wa ndani na nje.
“Malengo ya
sera ya madini 2009 pamoja mambo mengine ila muhimu wa kuifunganisha na sekta
zingine za kiuchumi ili kuchochea ukuaji wa sekta zingine na kuchangia
maendeleo ya taifa, alisema Mbibo
Kwa upande
wake, Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Madini na Biashara kutoka Tume ya Madini, CPA,
Dkt Venance Kasiki, alisema kwamba watanzania wanayo fursa ya kwenda kwenye
mgodi wa Buzwagi ambao upo kwenye hatua za mwisho za ufugaji.
“Hii ni
fursa ya kipekee kwa watanzania wazawa kwenda kwenye eneo la Buzwagi ambapo
kuna miundombinu bora na ya kisasa kama vile maji, umeme na Barabara kwa ajili
ya kufanya uwekezaji,” alisema Dkt CPA Kasiki
Alisema
kwamba eneo la mgodi wa Buzwagi watanzania wanaweza kuanzisha viwanda vya
bidhaa kwa ajili ya kuhudumia migodi kadhaa ya hapa nchini na kutokana na eneo
la Buzwagi ambalo lina Hecta
Alisema
kwamba pamoja na mambo mengine eneo la Buzwagi lenye hecta 3365 ambalo ni
maalum kama Kongani ya uwekezaji na viwanda (BSEZ) ina fursa ya zaidi ya
kujengwa sio tu viwanda vya bidhaa kwa ajili ya migodini hata viwanda vya
vipuri kwa ajili ya mitambo ya migodini.
Alisema
kwamba hii ni fursa ya kipekee kwa watanzania kuendelea kuunganisha nguvu zao
kutokana na miundombinu mizuri na bora kwenye eneo la Buzwagi ni kuharakisha
uanzishwaji wa viwanda na kutoa na kutoa bidhaa zenye ubora na viwango.
Dkt CPA
Kasiki alisema kwamba Tume hiyo imeendelea kutoa mafunzo na elimu kwenye
makampuni, taasisi za elimu mbalimbali na jamii kwa ujumla ili uelewa wa
Maudhui ya Ndani (Local Content) ili watanzania wapate uelewa zaidi kuhusu
kanuni hiyo.
“Serikali
kupitia Tume ya Madini imejikita na ina wataalamu wa kutosha wa kutoa elimu
kuhusu Maudhui ya Ndani (Local Content) ili watanzania waweze kupata uelewa na
kuingia kwenye sekta ya madini kwa ajili ya kupata kazi za kutoa huduma, ajira
na ukandarasi wa shughuli mbalimbali kwenye migodi ambayo ipo hapa nchini,”
aliongeza Dkt CPA Kasiki
Aliongea
kwamba ni umuhimu kwenye hii ushirikishwaji wa watanzania kwenye sekta ya
madini moja ya nyenzo muhimu ni ya kuungana (Joint venture) kwa maana ya
kutunisha mtaji ili kuweza kupata kazi kwenye migodi iliyopo hapa nchini.
Dkt CPA
Kasiki alifafanua kwamba serikali iliamua kuja na kanuni ya Maudhui ya Ndani
(Local Content) baada ya kilio cha umma (Public Outcry) kuhusu kwa watanzania
hususani jamii inayozunguka migodi kutokunufaika na uwepo wa rasilimali madini.
“Baada ya
kilio hicho cha muda mrefu na baadaye kuja kwa sera ya madini ya mwaka 2009 ya
kuwawezesha watanzania wazawa kushiriki katika uchimbaji wa madini, kupata kazi
za ukandarasi, zabuni na kutoa huduma mbalimbali,” alisema Dkt Kasiki
Dkt CPA
Kasiki aliongeza kwamba pamoja na mambo mengine sheria ya madini 2019 na 2022
ili kuja ili kutatua matatizo na kero za ushirikishwaji wa watanzania kwenye
sekta ya madini ili kupanua wigo na utatuzi wa changamoto hizo.
Aliongeza
kwamba fursa za kukuza mnyororo wa thamani kwa watanzania kupitia sekta ya
madini ni kubwa na pamoja mambo mengine fursa za kazi kama vile, mitambo ya
migodini, Tehama, ujenzi wa viwanda vya kutoa bidhaa kwenye migodi, usafi na
ufuaji wa nguo, famasi na tiba na huduma ya chakula.
Mwenyekiti
wa Tume ya Madini, Dkt Janet Lekashigo alitoa wito kwa wadau kuendelea
kushiriki kwenye Jukwaa la madini ili kuleta na kuchochea fikra za nafasi ya
ushirikishwaji wa watanzania kwenye sekta ya madini nchini.
Dkt
Lekashigo alisema kwamba jukwaa hilo ni kuchochea fikra mpya na majadiliano ya
kitaaluma ili kuweza kusaidia watanzania kushiriki kwenye uchumi wa sekta ya
madini.
“Jukwaa hili la nne ni la majadiliano, mawazo na kuleta fikra Chanya ili kuchochea mabadiliko ya ushirikishwaji wa watanzania kwenye sekta ya madini ili waweze kunufaika na rasilimali za madini hayo kwenye maeneo yao,” alisema Dkt Lekashigo
Aliongeza
kwamba umuhimu wa Jukwaa hilo ni kuja pia na mapendekezo mbalimbali ya namna
bora ya kuwawezesha na kufungua milango ya watanzania wazawa kufanya kazi zaidi
za ukandarasi na zabuni kwenye migodi hapa nchini.
Dkt
Legashiko alisema kwamba Tume hiyo itaendelea kushirikiana na wadau wote kwenye
sekta ya madini hususani sekta binafsi kupitia Maudhui ya Ndani (Local content)
kuhakikisha dira ya madini ni maisha ni utajiri inakamilishwa kikamilifu kwa
kuwashirikisha watanzania wazawa kwenye sekta ya madini nchini.











No comments:
Post a Comment