Na Mwandishi
Wetu, Mwanza
Mwenyekiti
wa Tume ya Madini, Dkt Janet Lekashigo ametoa wito kwa wadau kuendelea
kushiriki kwenye Jukwaa la madini ili kuleta na kuchochea fikra za nafasi ya
ushirikishwaji wa watanzania kwenye sekta ya madini nchini.
Akizungumza
kwenye Jukwaa la nne la utekelezaji wa ushirikishwaji wa watanzania katika
sekta ya madini unaofanyika jijni Mwanza, Dkt Lekashigo alisema kwamba jukwaa
hilo ni kuchochea fikra mpya na majadiliano ya kitaaluma ili kuweza kusaidia
watanzania kushiriki kwenye uchumi wa sekta ya madini.
“Jukwaa hili
la nne ni la majadiliano , mawazo na kuleta fikra Chanya ili kuchochea
mabadiliko ya ushirikishwaji wa watanzania kwenye sekta ya madini ili waweze
kunufaika na rasilimali za madini hayo kwenye maeneo yao,” alisema Dkt
Lekashigo
Aliongeza
kwamba umuhimu wa Jukwaa hilo ni kuja pia na mapendekezo mbalimbali ya namna
bora ya kuwawezesha na kufungua milango ya watanzania wazawa kufanya kazi zaidi
za ukandarasi na zabuni kwenye migodi hapa nchini.
Dkt
Legashiko alisema kwamba Tume hiyo itaendelea kushirikiana na wadau wote kwenye
sekta ya madini hususani sekta binafsi kupitia Maudhui ya Ndani (Local content)
kuhakikisha dira ya madini ni maisha ni utajiri inakamilishwa kikamilifu kwa
kuwashirikisha watanzania wazawa kwenye sekta ya madini nchini.
Kwa upande
wake, Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Madini na Biashara kutoka Tume ya Madini, CPA,
Dkt Venance Kasiki, alisema kwamba Tume hiyo imeendelea kutoa mafunzo na elimu
kwenye makampuni, taasisi za elimu
mbalimbali na jamii kwa ujumla ili uelewa wa Maudhui ya Ndani (Local Content)
ili watanzania wapate uelewa zaidi kuhusu kanuni hiyo.
“Serikali
kupitia Tume ya Madini imejikita na ina wataalamu wa kutosha wa kutoa elimu
kuhusu Maudhui ya Ndani (Local Content) ili watanzania waweze kupata uelewa na
kuingia kwenye sekta ya madini kwa ajili ya kupata kazi za kutoa huduma , ajira
na ukandarasi wa shughuli mbalimbali kwenye migodi ambayo ipo hapa nchini,”
aliongeza Dkt CPA Kasiki
Alisema
kwamba ni umuhimu kwenye hii ushirikishwaji wa watanzania kwenye sekta ya
madini moja ya nyenzo muhimu ni ya kuungana (Joint venture ) kwa maana ya
kutunisha mtaji ili kuweza kupata kazi kwenye migodi iliyopo hapa nchini.
Dkt CPA
Kasiki alifafanua kwamba serikali iliamua kuja na kanuni ya Maudhui ya Ndani
(Local Content) baada ya kilio cha umma
(Public Outcry) kuhusu kwa watanzania hususani jamii inayozunguka migodi
kutokunufaika na uwepo wa rasilimali madini.
“Baada ya
kilio hicho cha muda mrefu na baadaye kuja kwa sera ya madini ya mwaka 2009 ya
kuwawezesha watanzania wazawa kushiriki katika uchimbaji wa madini , kupata
kazi za ukandarasi, zabuni na kutoa huduma mbalimbali,” alisema Dkt Kasiki
Dkt CPA
Kasiki aliongeza kwamba pamoja na mambo mengine sheria ya madini 2019 na 2022
ili kuja ili kutatua matatizo na kero za ushirikishwaji wa watanzania kwenye
sekta ya madini ili kupanua wigo na utatuzi wa changamoto hizo.
Aliongeza kwamba fursa za kukuza mnyororo wa thamani kwa watanzania kupitia sekta ya madini ni kubwa na pamoja mambo mengine fursa za kazi kama vile , mitambo ya migodini , Tehama , ujenzi wa viwanda vya kutoa bidhaa kwenye migodi, usafi na ufuaji wa nguo , famasi na tiba na huduma ya chakula.









No comments:
Post a Comment