KADA WA CCM NA MFANYABIASHA HAIDARY GULAMALI ACHUKUA FOMU KUWANIA UBUNGE JIMBO LA ILONGERO SINGIDA - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Sunday, June 29, 2025

KADA WA CCM NA MFANYABIASHA HAIDARY GULAMALI ACHUKUA FOMU KUWANIA UBUNGE JIMBO LA ILONGERO SINGIDA

KADA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na mfanyabiasha, Haidary Gulamali leo Juni 28, 2025 amechukua fomu ya kugombea Ubunge jimbo jipya la Ilongero.

...........................................

Na Dotto Mwaibale

KADA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na mfanyabiasha Haidary Gulamali leo Juni 28, 2025 amechukua fomu ya kugombea Ubunge jimbo jipya la Ilongero lililopo Wilaya ya Singida kupitia CCM ambapo atapambana na Mbunge aliyemaliza muda wake, Ramadhani Ighondo, anayetetea nafasi   hiyo.

Wagombea wengine ambao wametajwa kuwania nafasi hiyo ni  Rehema Maji, Rozalia Kitiku, Alfred Ringi, Ramadhani Mdoe, Maulid Sombi na Mercy Mumbee.

2.       Wengine ni Abdallah Haji, Chrisogone Mangi, Hashim Ntandu, Gloria Nkungu, Musa Kuji, Juma Sima, Lazaro Nyalandu na Amani Nyekele.

3.       Wengie wanaotajwa ni Huruma Kilakuno, Baraka Musa, Sabasaba Manase, Juma  Ng’imba, Dr. Khalid Salla, Tatu Mohamed Kisija, Haruna Ntandu na Samson Mtaturu, Haidary Gulamali na Japhet Mungwe.

Kati ya wagombea hao Gulamali anauzoefu kwa kiasi kikubwa kwani awamu hii ni ya pili kugombea nafasi hiyo muhimu ya kuwatumikia wananchi.

Katika jimbo hilo Serikali imefanya kazi kubwa ya maendeleo chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia mbunge aliyemaliza muda wake, Ramadhani Ighondo lakini kutokana na kuwepo kwa demokrasia ndio maana wamejitokeza wagombea wengi kuwania nafasi hiyo ili atakayefanikiwa kuwa mbunge aweze kuendeleza  maendeleo zaidi kwenye maeneo  ambayo bado yana changamoto kama vile kwenye sekta ya elimu, afya, barabara, umeme, kilimo, ufugaji utunzaji wa mazingira  na mengineyo.

Jimbo jipya la Ilongero ili lipige hatua kubwa ya maendeleo linahitaji viongozi  wenye uwezo mkubwa wa kuwaondoa wananchi kwenye umasikini kwa kusimamia vizuri ilani ya uchaguzi ya 2025/ 2030 baada ya  2020/ 2025 kufanya vizuri.    

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad