MBOBEZI WA MASUALA YA UGAVI, GWATENGILE ACHUKUA FOMU KUPAMBANA NA ATUPELE MWAKIBETE JIMBO LA BUSOKELO - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Saturday, June 28, 2025

MBOBEZI WA MASUALA YA UGAVI, GWATENGILE ACHUKUA FOMU KUPAMBANA NA ATUPELE MWAKIBETE JIMBO LA BUSOKELO


Mtia nia wa ubunge Jimbo la Busokelo, Ezekiel Mwakyambo Gwatengile akionesha fomu ya kugombea nafasi hiyo baada ya kukabidhiwa Juni 28, 2025 katika ofisi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tukuyu wilayani Rungwe.
......................... 

Na Dotto Mwaibale

MTAALAMU wa Masuala ya  ugavi, ununuzi na masoko  Ezekiel Mwakyambo Gwatengile tayari amechukua fomu ya kugombea Ubunge jimbo la Busokelo lililopo Rungwe mkoani Mbeya kupitia Chama Cha Mapinzuzi (CCM), ambapo atapambana na Mbunge aliyemaliza muda wake, Atupele Mwakibete anayetetea nafasi   hiyo.

Wagombea wengine ambao wametajwa kuwania nafasi hiyo ni aliyekuwa mkuu wa mkoa mstaafu wa Kigoma, Thobias Andengenye,, Wakili Gerald Mwayonde na Lutengano Mwalwiba.

Gwatengile anauzoefu wa uongozi kwani amewahi kushiriki makongamano mbalimbali ya  kitaifa na kimataifa, amewahi kuwa Mwenyekiti wa UVCCM Tawi, Mjumbe Mwakilishi wa CCM Wilaya, na sasa anahudumu kama Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Mbeya hadi mwaka 2027. Pia ni Mwenyekiti wa BUDEA, KAMBADEA na UKUKIKAMA jijini Dar es Salaam, hivyo kuwa na mchango mkubwa katika ustawi wa jamii.

Katika jimbo hilo Serikali imefanya kazi kubwa chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia mbunge aliyemaliza muda wake, Atupele Mwakibete, lakini kutokana na kuwepo kwa demokrasia watia nia hao wa nafasi hiyo wamejitokeza ili atayefanikiwa kuwa mbunge aweze kuendeleza  maendeleo zaidi kwenye maeneo  ambayo bado yana changamoto kwenye sekta ya elimu, afya, barabara, umeme, kilimo na mengineyo.

Jimbo la Busokelo linahitaji kupata viongozi wenye uwezo, maono na ubunifu ili liweze kupiga hatua kubwa ya maendeleo na kutekeleza kwa vitendo ilani ya uchaguzi ya 2025/ 20230.

Mtia nia huyo Gwatengile akionesha ishara ya miaka mitano tena kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Mtia nia huyo Gwatengile akijaza fomu hiyo baada ya kukabidhiwa.
Mtia nia huyo Gwatengile akikabidhiwa fomu hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad