.........................................
Na Mwandishi Wetu
Katika siku za karibuni, taifa letu limejikuta likikumbwa na wimbi la taarifa za uzushi, upotoshaji na uvunjifu wa maadili ndani ya taasisi za umma, ikiwemo mchakato nyeti wa kuchuja majina ya watia nia wa nafasi za udiwani na ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM). Tabia hiyo si tu inakera, bali pia inatishia misingi ya uwajibikaji, nidhamu na uzalendo ambayo taifa letu limeijenga kwa muda mrefu kwa jasho na hekima ya viongozi wetu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa busara yake ya kipekee, amekuwa akisisitiza kwa nguvu suala la maadili na uzalendo kwa watumishi wa umma. Katika hotuba yake ya Mei 24, 2025, alieleza kwa uchungu na kwa ukali unaostahili jinsi ambavyo baadhi ya watumishi wa umma wamepotoka — siyo tu kwa kukosa maadili ya kazi, bali pia kwa kutotambua wajibu wao kwa taifa.
Alisema kwa uchungu: “Mtumishi anathubutu kuchukua siri kwenye mafaili, kupiga picha kwa simu yake na kusambaza… Yeye ndiye aliyekosa maadili, yeye ndiye asiyewajibika kwa taifa lake.” Kauli hii ni nzito. Inatufunua macho kuwa chanzo kikuu cha baadhi ya migogoro ya kisiasa na kiutendaji serikalini ni kushuka kwa maadili, kukosekana kwa uaminifu na kuachwa kwa misingi ya uzalendo.
Kwa kujua zaidi taarifa za watia nia hao kudaiwa kuvuja na kusambaa katika mitandao ya kijamii kabla ya wakati ambapo zilipaswa kutolewa na idara ya uenezi ya CCM Taifa na hatua zinazopaswa kuchukuliwa pitia ueneziccm.blogspot.com.









No comments:
Post a Comment