KANUNI HAZIJAKIUKWA CCM KUFANYA MKUTANO KWA NJIA YA MTANDAO - SINGIDANIBLOG

Habari za Hivi Punde

Post Top Ad

Saturday, July 26, 2025

KANUNI HAZIJAKIUKWA CCM KUFANYA MKUTANO KWA NJIA YA MTANDAO

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan (katikati), akiwa pamoja na viongozi mbalimbali wakati wa Mkutano Maalum wa chama hicho uliofanyika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete (JKCC) Jijini Dodoma Mei 29,2025.

............................ 

Na Dotto Mwaibale

JANA Julai 25, 2025 Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM  Taifa  (NEC), Itikadi na Mafunzo, Amos Makalla aliutangazia umma kupitia vyombo ya habari kwamba chama hicho leo Julai 26, 2025 kitafanya mkutano mkuu maalumu kwa njia ya mtandao.

Mara baada ya tamko hilo la Makalla kumekuwa na maneno mengi kutoka kwa baadhi ya wananchi wakihoji  ni kwanini chama hicho kinafanya mkutano kwa njia hiyo kwa sababu jambo hilo halijazoeleka.

Hata hivyo, kufanya mikutano kwa njia ya mtandao ni jambo ambalo limeanza siku nyingi duniani na limekuwa likisaidia kupunguza gharama kwani kufanyika kwa mikutano wa njia hiyo  mtu anaweza kushiriki mkutao husika akiwa eneo lolote alipo.

Lakini hoja ya baadhi ya wananchi wanaona  jambo hilo  ni kama limekiukwa na chama hicho kitu ambacho sio cha kweli kwani CCM iliona mbali na ndio maana katika katiba yake iliyofanyiwa maboresho ilianisha kuwa kunaweza kufanyika mikutano ya chama  kwa njia ya mtandao.

Ni kwa msingi huo wanaohoji suala hilo  kwamba kanuni zimekiukwa  hawana hoja na wanapaswa kuisoma katiba ya chama hicho Toleo la Mei 2025 ibara ya 99 (i) na (ii) A - F inaeleza vikao vilivyoorodheshwa kwenye (i) vinaweza kuendeshwa kwa njia ya Mtandao kama kuna ulazima wa kufanya hivyo.

Vikao hivyo ni Mkutano Mkuu wa CCM Taifa, Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Sekretarieti ya Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Zanzibar, Kamati ya Wabunge Wote wa CCM, Kamati ya Wajumbe wote wa Baraza la Wawakilishi wa CCM Zanzibar.

Hatua hiyo ya CCM kufanya mkutano huo kwa njia ya mtandao huenda imelenga kupunguza gharama na muda ambao ungetumika hasa kwa kuzingatia chama kina mambo mengi ya kufanya ukiwepo mchakato wa kupitisha majina ya watia nia waliomba ridhaa ya kuwania nafasi ya udiwani na ubunge.

Makala alisema maandalizi ya mkutano huo utakaofanyika leo tayari yamekamilika na kuwa moja ya ajenda yake kuu ni kufanya marekebisho madogo kwenye katiba.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad