Mtia nia wa ubunge wa Jimbo la Kivule kupitia Chama Cha ACT Wazalendo, Colman Obote Marwa akitangaza nia ya kugombea nafasi hiyo.
.......................................
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
WANANCHI Jimbo la Kivule wamemtwisha mzigo mtia nia wa ugombea ubunge katika jimbo hilo kupitia Chama cha ACT Wazalendo Colman Obote Marwa wakimtaka akichaguliwa kipaumbele chake cha kwanza kiwe ni ujenzi wa barabara ya Kivule Msongola.
Ombi hilo lilitolewa na wananchi hao hivi karibuni wakati wa hafla ya kuzaliwa kwa mtia nia huyo ambayo alitumia hafla hiyo kutangaza nia ya kugombea nafasi hiyo kwa lengo la kuwatumikia wananchi wa jimbo hilo.
“Ndugu yetu Colman tunakufahamu vizuri kwani unauzoefu na uongozi tunachokuomba ukipata nafasi hiyo kipaumbele cha kwanza kiwe ni ukamilishaji ujenzi wa hii barabara ya Kivule kwenda Msongola kuanzia hapa relini,” alisema mmoja wa wananchi aliyekuwepo kwenye hafla hiyo.
Mwenyekiti wa Uchaguzi wa Jimbo hilo jipya la Kivule kupitia chama cha ACT Wazalendo, Abilahi Alifa alisema chama hicho kimejipanga vizuri kuhakikisha mtia nia huyo anashinda na kuwa mbunge wa jimbo hilo ambalo linachangamoto nyingi za kijamii ambazo zimetokana na kusahulika kwa muda mrefu ambapo alimtakia safari ya mafanikio.
Mtia nia huyo Colman Marwa akizungumza kwenye hafla hiyo alisema anawiwa kuwatumikia wananchi wa jimbo hilo na kuhakikisha anafanya mapinduzi makubwa ya maendeleo bila ya kubagua watu kwa itikadi za vyama vyao.
Colman Marwa ni mkazi wa eneo hilo la Kivule kwa muda mrefu na ni mzoefu wa uongozi kwani mwaka 2014 alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Serikali wa Mtaa wa Yangeyange Kata ya Msongola kupitia Chama cha Wananchi CUF ambapo pia mwaka 2015 alijitosa kugombea ubunge na udiwani kupitia CUF.
Safari hii tena Marwa ametia nia ya kugombea nafasi hiyo ya ubunge jimbo la Kivule na Udiwani Kata ya Msongola.
Mama wa Mtia nia huyo, Bibi Yulita Gimonge akitambulishwa kwenye hafla hiyo.Baadhi ya viongozi wa ACT Wazalendo Jimbo la Kivule wakiwa kwenye hafla hiyo.
Wageni waalikwa wakipata msosi kwenye hafla hiyo.
Matukio mbalimbali kwenye hafla hiyo
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye mkutano huo.
Mama wa mgombea nafasi hiyo akipongezwa.
Viongozi wa Chama Cha ACT Wazalendo wakiwa kwenye hafla hiyo.







No comments:
Post a Comment