DK. KAZOBA AWAVUTIA WADAU TIBA ASILI DODOMA, AINGIA KWA MBWEMBWE KAMA RAIS TRAORÉ

Subscribe Us

DK. KAZOBA AWAVUTIA WADAU TIBA ASILI DODOMA, AINGIA KWA MBWEMBWE KAMA RAIS TRAORÉ

Mkurugenzi Mkuu wa Kazoba International Herbal Products, Dk. Kazoba, akizungumza na mmoja wa wananchi aliyetembelea banda la kampuni hiyo huku akinogesha kwa kuvaa mfano wa mavazi rasmi ya kijeshi yanayovaliwa na Rais wa Burkina Faso, Ibrahim TraorĂ©  kwenye maonesho ya Wiki ya Tiba Asili ya Mwafrika yanayoendelea katika viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma . 

,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

Godwin Myovela, Dodoma

Maonesho ya Wiki ya Tiba Asili ya Mwafrika yanayoendelea katika viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma leo yalipata sura mpya ya aina yake baada ya Mkurugenzi Mkuu wa Kazoba International Herbal Products, Dk. Kazoba, kuwasili kwa mbwembwe akiwa amevalia mfano wa mavazi rasmi ya kijeshi yanayovaliwa na Rais wa Burkina Faso, Ibrahim Traoré.

Tukio hilo liliibua msisimko mkubwa, ambapo mamia ya wataalamu wa tiba asili na wananchi walilipuka kwa shangwe mara msafara wake ulipoingia viwanjani, ukisindikizwa na mabaunsa kadhaa waliotia chachu katika shamrashamra hizo.

Baada ya kusalimiana na washiriki wa maonesho alipokuwa akipita banda moja hadi jingine, Dk. Kazoba aliteka hisia za umati, huku wengi wakionesha kuvutiwa na haiba yake, umaridadi wa mavazi yake na ujasiri aliouonesha.

Akizungumza na waandishi wa habari, Dk. Kazoba alitumia nafasi hiyo kutambulisha huduma na bidhaa mpya alizozileta mwaka huu, ikiwemo Kazoba Energy Drink, pamoja na dawa mbalimbali zenye lengo la kutoa tiba kwa maradhi yanayoisumbua jamii.

“Kazoba International Herbal Products imejikita katika kuhakikisha kila mwananchi anapata tiba salama na yenye matokeo chanya. Tiba zetu asili ni matokeo ya utafiti, na zimedhihirisha uwezo wa kutatua changamoto nyingi za kiafya,” alisema kwa msisitizo.

Alifafanua kuwa bidhaa hizo zimekuwa msaada kwa wagonjwa wanaokabiliwa na maradhi sugu kama kansa, shinikizo la damu, kisukari, magonjwa ya mifupa na viungo, vidonda vya tumbo, pamoja na matatizo ya kupumua kama homa ya mapafu na pumu ya ngozi.

Akiongeza kwa uthabiti, alisema tiba hizo pia zina suluhisho kwa tezi dume, henia, bawasiri, ganzi, malaria sugu, miguu kuwaka moto, matatizo ya nguvu za kiume, kushuka kwa hamu ya tendo la ndoa, na changamoto za uzazi.

“Tunapambana kuondoa dhana kwamba tiba asili haina nafasi ya kisayansi. Leo hii tuna ushahidi wa kitaalamu kwamba tiba hizi zinasaidia, zinaponya na kuokoa maisha,” alieleza Dk. Kazoba.

Aidha, aliwaalika wakazi wa Dodoma na mikoa jirani kufika kwenye banda lao kupata huduma hizo, akibainisha kuwa ofisi za Kazoba International Herbal Products zipo pia katika majiji ya Dar es Salaam, Arusha, Mwanza na Dodoma.

Kwa kauli mbiu ya mwaka huu, “Tuimarishe Huduma za Tiba Asili zenye Ushahidi wa Kisayansi,” ushiriki wa Dk. Kazoba si tu umeongeza hamasa ya kitaifa kuhusu tiba asili, bali pia umetia chachu ya mjadala mpana juu ya nafasi ya tiba asili katika kulinda afya na ustawi wa jamii ya Watanzania.

Maeezo yakitolewa kwenye kwenye maonesho ya Wiki ya Tiba Asili ya Mwafrika yanayoendelea katika viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma.
Wananchi waliotembelea mabanda katika maonesho hayo wakipata maelezo kuhusu bidhaa za Tiba Asili kwenye maonesho hayo.
Bidhaa Tiba Asili zikinadiwa kwenye maonesho hayo.
Mkurugenzi Mkuu wa Kazoba International Herbal Products, Dk. Kazoba,  akiwa katika picha ya amoja na wafanyakazi wa Kampuni ya Kazoba na walinzi wake binafsi. "Baunsa"
Picha ya pamoja.
 

Post a Comment

0 Comments