Na Godwin Myovela, Dodoma
Taasisi ya Golden Star Enterprises, yenye makao yake makuu jijini Arusha, imewasili kwa kishindo kwenye maonesho ya Wiki ya Tiba Asili ya Mwafrika yanayoendelea katika viwanja vya Chinangali Park jijini Dodoma, ikiwaletea wananchi tiba na kinga bora zitokanazo na mimea na matunda ya asili.
Akizungumza kwenye banda lao, Mkurugenzi Mkuu wa taasisi hiyo, Dk. Mussa James Daudi, amesema Golden Star imejikita katika kutoa suluhisho la uhakika kwa magonjwa sugu na yasiyo sugu, ambayo kwa muda mrefu yamekuwa mzigo mkubwa kwa jamii.
“Tunatoa tiba na kinga za uhakika kwa maradhi kama vidonda vya tumbo, bawasiri, UTI, PID (maambukizi kwenye via vya uzazi vya wanawake), aleji, kifua aina zote, gout, chango kwa akinamama na akina baba, ngiri, tezi dume, typhod, malaria na magonjwa ya zinaa. Pia tunasaidia wagonjwa wenye presha kwa kutoa huduma za kukoturo presha, kuimarisha mishipa ya damu, kuondoa sumu mwilini (detox) pamoja na kusafisha mishipa ya damu ili kurudisha afya njema ya moyo na mwili kwa ujumla,” alisema Dk. Mussa.
Kwa upande wake, Meneja Mkuu wa Golden Star, Dk. Jackline Mollel, amewakaribisha wananchi kwa wingi kutembelea banda lao na kusisitiza kuwa huduma wanazotoa zimejikita kwenye ushahidi wa kisayansi sambamba na kaulimbiu ya mwaka huu:
“Tuimarishe Huduma za Tiba Asili zenye Ushahidi wa Kisayansi.”
Mbali na tiba, Golden Star pia inatoa huduma za massage za kitaalamu, kuimarisha kinga kwa kuongeza CD4, kutoa usaidizi katika matatizo ya mishipa ya fahamu, kusafisha cholesterol mwilini, na ushauri wa kitaalamu wa kiafya kuhakikisha wagonjwa wanapata nafuu ya haraka na kurejea kwenye afya bora.
“Tunawaambia wananchi wote wa Dodoma na mikoa jirani—msikose fursa hii. Banda letu liko wazi kwa kila mmoja, tunatoa huduma kwa bei nafuu na matokeo ya haraka. Baada ya maonesho, tunapatikana pia Arusha kwenye makao makuu yetu kwa huduma endelevu,” alisisitiza Dk. Jackline.
0 Comments