.................................
Na Dotto Mwaibale
Mgombea nafasi ya Urais Kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kesho Agosti 29, 2025 anatarajia kuzungumza (kuunguruma) na Wanachama wa CCM, Wananchi wa Mkoa wa Morogoro katika mkutano wake wa kwanza wa kampeni baada ya kuzindua kampeni hiyo kitaifa leo Agosti 28, 2025.
Katika mkutano huo atautumia kwa ajili ya kuzungumza nao mambo mbali ya maendeleo na kuinadi Ilani ya CCM 2025 - 2030 ikiwa na kuomba kupigiwa kura nyingi wagombea wote wa CCM kuanzia mgombea wa Urais, Mbunge na Diwani.
Rais Samia atakuwa kwenye kampeni mkoani humo kwa siku mbili Agosti 29 na 30, 2025.
0 Comments