DKT. SAMIA : KUPITIA FALSAFA YA R4 TUMEIHESHIMISHA TANZANIA NDANI YA BARA LA AFRIKA NA DUNIA

Subscribe Us

DKT. SAMIA : KUPITIA FALSAFA YA R4 TUMEIHESHIMISHA TANZANIA NDANI YA BARA LA AFRIKA NA DUNIA

Mgombea nafasi ya Urais kupitia CCM Dkt. Samia Suluhu Hassan

.............................................

Na Mwandishi Wetu  

Mgombea nafasi ya Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt.Samia Suluhu Hassan amesema       kupitia falsafa ya R4 Tanzania tumeiheshimisha ndani ya Bara la Afrika na Duniani.

Dkt. Samia ameyasema hayo wakati akizindua kampeni za uchaguzi mkuu wa 2025 wa chama hicho uliofanyika viwanja vya Tanganyika Packers Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na mgombea mwenza Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi. 

" Kupitia falsafa ya R4 , tulihakikisha Taifa linaendelea kuwa na heshima ndani ya Bara la Afrika na duniani kwa kutunza amani na utulivu na ripoti ya Global Peace Index ya mwaka huu 2025, inaonesha kuwa Tanzania inaongoza kwa viwango vya amani ndani ya ukanda wa Afrika Mashariki,” alisema.

Post a Comment

0 Comments