Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa uzinduzi wa Kampeni za chama hicho Agosti 28,2025 Jijini Dar es Salaam.
...........................................
Chama cha Mapinduzi (CCM) leo kimeandika ukurasa mpya katika historia ya siasa za Tanzania baada ya kuzindua rasmi kampeni zake za Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025. Tukio hili, linalofanyika katika Viwanja vya Tanganyika Packers jijini Dar es Salaam, limebeba hamasa ya kipekee, kwani mgombea urais wa CCM na Mwenyekiti wa chama hicho, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, amepokea rasmi kijiti cha kuongoza mbio za ushindi.
Kabla ya kuelekea uwanjani, Rais Samia alifanya dua maalum Ikulu jijini Dar es Salaam, akimkabidhi Mwenyezi Mungu jukumu la kuomba ridhaa ya wananchi kwa awamu ya pili. Dua hiyo imeonesha unyenyekevu na heshima yake kwa taifa na kwa imani za Watanzania wote, ishara kuwa safari ya kampeni hizi inalenga mshikamano, amani na mshindi wa kheri...SOMA ZAIDI
0 Comments