MTANDAO WA BLOGU TANZANIA WAHIMIZA AMANI UCHAGUZI MKUU 2025

Subscribe Us

MTANDAO WA BLOGU TANZANIA WAHIMIZA AMANI UCHAGUZI MKUU 2025

Mwenyekiti TBN, Beda Msimbe

................................................... 

Mtandao wa Wanablogu Tanzania (TBN) umewataka wagombea wa vyama vya siasa na wananchi kwa jumla kudumisha amani na mshikamano kabla na baada ya Uchaguzi Mkuu, hususan katika kipindi hiki cha kampeni za uchaguzi huo.


Taarifa iliyotolewa Agosti 28, 2025 na Mwenyekiti wa TBN Beda Msimbe, kwenda kwenye vyombo vya habari, imesema, TBN inasisitiza kuwa utunzaji wa amani ni jukumu la kila mmoja, huku akihimiza vyama vya siasa kuendesha kampeni bila kuhatarisha mshikamano wa kitaifa.


“Tunaomba vyama vyote vya siasa vitumie kipindi hiki kueleza ilani zao kwa wananchi kistaarabu na bila kuhatarisha amani tuliyonayo...SOMA ZAIDI

Post a Comment

0 Comments